WAZIRI wa Afya, Maendeleo
ya Jamii Jinsia,Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu katikati akimkabidhi vifaa vya michezo ambavyo ni
viatu Mwenyekiti wa timu ya African Sports
Awadhi
Salehe Pamba ikiwa ni kuipa motisha timu hiyo kufanya vizuri kwenye
michuano wanayoshiriki ili waweze kufanya vizuri na hatimaye kuweza
kurejea daraja la kwanza na Ligi kuu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya
ya Tanga,Meja Hamisi Mkoba
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya
Jamii Jinsia,Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu kushoto akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Klabu ya
African Sports Awadhi Salehe Pamba leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mara
baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo
WAZIRI wa
Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Mwenyekiti wa Klabu ya
African Sports Awadhi Salehe Pamba leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mara
baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kushoto ni
Mwenyekiti wa
CCM wilaya ya Tanga,Meja Hamisi Mkoba
Halfa ya makabidhiano
ikiendelea
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi viatu hivyo Nahodha wa timu ya African Sports Mohamed Kidiwa |
NA MWANDISHI
WETU, TANGA.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya
Jamii Jinsia,Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu ametoa vifaa vya michezo kwa timu ya African Sports ya
Tanga yenye thamani ya zaidi ya milioni 1.5 ikiwa ni mkakati kabambe wa
kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki na
hatimaye kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Makabidhiano hayo yalifanyika
leo kwenye uwanja wa CCM
Mkwakwani mjini Tanga wakati wa ufunguzi wa timu ya wanawake ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) ya wilaya ya Tanga ambapo alisema vifaa hivyo vitakuwa ni
chachu ya timu hiyo kuweza kufikia malengo yao.
Aliyasema hayo mara baada ya
kukabidhi vifaa hivyo kwa timu
hiyo katika halfa iliyoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa klabu ya
African Sports ambapo alisema dhamira yake kubwa ni kuhakikisha timu hiyo
inarejea ligi daraja la kwanza na ile ya Coastal Union ihakikisha msimu ujao
inarudi Ligi kuu.
“Niseme tu sisi tumejipanga
kuhakikisha tunazirejesha timu
hizi kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara tukianzia na timu ya
Coastal Union lakini ndugu zangu African Sports mhakikishe mnarudi ligi daraja
la kqwanza na baadae ligi kuu “Alisema
Akizungumza baada ya kupokea
vifaa hivyo,Mwenyekiti wa Klabu
ya African Sports,Awadhi Salehe Pamba alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia
msaada huo ambao utakuwa ni chachu kwao kuweza kufikia malengo yao kutokana na
changamoto hiyo kwisha.
Alisema msaada uliotolewa na
Waziri utakuwa chachu kubwa
kwao kuweza kufikia malengo yao waliojiwekea ya kuhakikisha wanarudi ligi kuu
kwani ndio ndoto yao kubwa ambayo wamekuwa wakiiwaza kila
wakati.
“Mh Waziri tukushukuru sana
katika hili umetupa nguvu ya
kuweza kupambana na tuna kuhaidia kuhakikisha tunairudisha timu Ligi daraja la
kwanza na hatimaye ligi kuu.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya
Tanga Raha)
No comments:
Post a Comment