WAZIRI wa Afya, Maendeleo
ya Jamii Jinsia,Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga kushoto
akikabidhi fedha
taslimu milioni 3 na nusu kwa ajili ya mishahara ya wachezaji wa timu
ya Coastal Union ya mwezi Desemba na
gharama za chakula kwa moja ya viongozi katikati anayeshughudia ni
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union Salim
Bawaziri.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga kushoto
akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga(TRFA) Said
Soud wakati alipotembelea kambi ya timu ya Coastal Union eneo la
Saruji jijini Tanga leo
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga wa nne
kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya
Coastal Union mara baada ya kutembelea kambi yao na kuwakabidhi fedha
za mishahara kwa uongozi wa timu hiyo kwa ajili ya
wachezaji
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na
Watoto,Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga leo January 5 mwaka
2018 ametembelea kambi ya timu ya Coastal Union iliyopo eneo la Saruji Jijini
Tanga ambayo hivi sasa inashiriki ligi daraja la kwanza na ipo nafasi ya tatu
kwenye kundi B.
Mh Ummy akizungumza wakati
alipoitembelea amewataka wachezaji wa timu hiyo kuongeza jitihada na
kujituma ili kushinda mechi nne zilizobakia kwa lengo la kujihakikishia nafasi
ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa mwaka
2018/2019.
“Coastal Union ikipanda daraja
na kucheza Premier League sio
tu itawezesha vijana kupata kipato bali pia itachochea uchumi na maendeleo ya
Jiji la Tanga “Alisema Waziri Ummy.
Katika kuhamasisha huko Mhe
Waziri Ummy amekabidhi shilingi
milioni 3 na nusu kwa ajili ya mishahara ya wachezaji ya mwezi Desemba na
gharama za chakula huku akihaidi kutoa zawadi y ash.milioni 2 kwa kila mechi
watakayoshinda kati ya mechi nne zilizobaki.
Wakizungumza wakati wa tukio
hilo,Kocha Mkuu wa timu ya
Coastal Union Juma Mgunda
amemuhakikishia Mh Ummy kuwa vijana wapo tayari kwa ushindi na hivyo anaamini
hawatamuangusha katika michezo yao hiyo iliyosalia katika michuano ya Ligi
Daraja la kwanza.
Aidha pia wameshukuru Mh Ummy
kwa kujitoa kwake ili
kuhakikisha timu hiyo inapanda daraja ambapo tukio hilo la makabidhiano
limehudhuriwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tanga (TRFA)
Said Soud na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union Salim
Bawaziri.
(Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
(Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
No comments:
Post a Comment