Kaimu Mkurugenzi wa BoT, Tawi la Mtwara, Bi. Leticia Rweyemamu, akitoa hotuba ya kufunga semina ya sikju tano ya waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha, kwenye makao makuu ya tawi hilo Mkoani Mtwara leo Ijumaa Februari 9, 2018.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mtwara
SEMINA ya siku tano ya waandishi wa Habari
za Uchumi, Biashara na Fedha iliyoandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania, Idara ya Uhussiano na Itifaki, imemalizika leo Februari 5, 2018 mkoani Mtwara.
Katika simian hiyo iliyofunguliwa mwanzoni
mwa wiki na Naibu Gavana wa Benki Kuu anayeshughulikia Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC), Bw.
Julian Raphael Banzi, waandishi hao wamejifunza mambo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na mabadiliko ya mfumo mpya wa kuandaa Sera ya Fedha, (Financial
Monetary Policy), mapitio ya maendeleo ya uchumi nchini, kikanda na dunia,
mifuko ya dhamana kwa wajasiriamali na dhamana za serikali.
Mambo mengine ambayo waandishi hao kutoka
vyombo mbalimbali vikiwemo, Redio, Luninga, Magazeti na Blogs ni kanuni mpya za
usimamizi wa bureaux de change, usimamizi wa mabenki na taasisi za fedha na
dhamana kwa mikopo ya nyumba (Mortgage Finance).
Waandishi hao pia wamepata wasaa wa
kujifunza nafasi ya matawi ya BoT katika utekelezaji wa majukumu ya benki hiyo,
fidia za interoperability katika kukuza huduma rasmi za fedha ili kujua
kuna usalama gani wa fedha za wateja wanaotumia mifumo ya kufanya miamala ya
kampuni za simu.
Lakini pia wamejifunza kuhusu nafasi ya
dodi ya ya amana katika ufilisi na kwa nini ulipaji fidia kwa wateja wa benki
zilizofilisiwa unachukua muda mrefu, mafanikio na changamoto katika utekelezaji
wa Sera ya Fedha Safi (Clean Money Policy), mafanikio na changamoto za dawati
la kutatua malalamiko ya wateja wa benki na taasisi za fedha.
Aidha waandishi hao pia walipata fursa ya
kutembelea miradi ya kiuchumi inayotekelezwa na serikali na taasisi binafsi ya
uchimbaji na uc hakataji wa gesi, huko Mnazi-Bay na Madimba.
Akifunga semina hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa
BoT tawi la BoT, Mkoani Mtwara, Bi. Leticia Rweyemamu, amewataka waandishi hao
kutumia elimu waliyoipata ili kuhabarisha umma kwa usahihi kuhusu kazi za Benki
Kuu, na kutumia faida waliyopata ya kukutana na wataalamu mbalimbali wa BoT ili
wawatumie kupata ufafanuzi wa habari mbalimbali za kiuchumi ili kuandaa habari
timilifu.
“Nimejifunza kutoka kwenu kwamba ubora wa
habari unategemea idadi ya watoa taarifa katika habari hiyo na ninatoa rai kuwa
watumieni wataalamu hao ipasavyo ili kuzifanya taarifa zenu kwa wananchi ziwe
bora zaidi.” Alisema Bi. Rweyemamu
Aitoa wito kwa waandishi hao kutumia
utaalamu kuelimisha umma kutumia huduma rasmi za kibenki ili kutunza fedha na
kufanya miamala kwani ni muhimu kwa sababu licha ya kuhakikisha usalama wa
fedha za mtyumiaji wa huduma hizo kuna uwezekano mkubwa wa kujikinga na upotevu
wa fedha unaoweza kutokea kwa sababu mbalimbalin ikiwemo wizi.
“Pia toeni uchambuzi wa kina kuhusu taarifa
za fedha, (Financial Statements), za mabenki na taasisi za fedha ili
kuwawezesha wananchi waliokuwa na amana au wangependa kuwekeza amana zao kuwa
na taarifa sahihi kuhusu hali ya taasisi hizo ili kufanya maamuzi sahihi.
“Haitoshi kuandika kuwa benki fulani
imepata faida kiasi Fulani au hasara kiasi Fulani tu, ni vema wananchi wakapata
taarifa mbalimbali zinazohusu ukwasi wa taasisi husimka, ikiwemo mali, madeni
pamoja na mipango mbalimbali ya taasisi hizo za kifedha.” Alifafanua.
Bi. Rweyemamu, amewahamasisha waandishi
hao kutumia nafasi ya BoT kuhabarisha namna inavyoandaa na kutekeleza sera ya
fedha ili kuhabarisha umma mwenendo wa uchumi na sekta ya fedha nchini ili
hatimaye wafanye maamuzi sahihi ya kuhusu uwekezaji hapa nchini.
Alivitaka vyombo vya habari kutumia nafasi
kubwa katika kutoa taarifa zinazochangia maendeleo ya uchumi wa viwanda na
kupunguza fursa kubwa inayotolewa kwa taarifa za kuburudisha tu, kwani kwa
kufanya hivyo vyombo vya bhabari vitaisaidia serikali kuelezea mipango yake ya
kueldekea uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.
“Kama alivyoeleza Naibu Gavana wakati
akifungua semina hii, Benki Kuu inatambua mchango wa vyombo vya ahabari vyote
ikiwemo redio, televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii katika kutangaza
habari za benki hiyo kwa manufaa ya umma.”
Kwa upande wake, Kaimu Meneja Uhusiano na
Itifaki wa BoT, Bi. Vicky Msina alisema BoT itaendelea kutoa mafunzo kwa
waandishi wa habari kwani kwa kufanya hivyo kunajenga uwezo wa waandishi
kufanya uchambuzi wa taarifa mbalimbali na kuziandika kwa usahihi.
“Nimefarijika sana kuwa pamekuwepo na
uelewa mkubwa wa waandishi hawa kuhusu utekelezaji na majukumu ya Benki Kuu.”
Alisema
Kaimu Meneja wa Idara ya Uhusiano na Itifaki, BoT, Bi. Vicky Msina, akizungumza wakati wa hafla ya ufungaji wa semina hiyo.
Dkt. Suleiman Missango, Meneja Msaidizi-Idara ya Utafiti, Kurugenzi ya Sera za Uchumi na Utafiti, BoT, akiwasilisha mada kuhusu Government
securities (Government Date Securities) , mwishoni mwa semina hiyo leo Februari 9, 2018.
Dkt. Suleiman Missango, Meneja Msaidizi-Idara ya Utafiti, Kurugenzi ya Sera za Uchumi na Utafiti, BoT, akiwasilisha mada kuhusu Government
securities (Government Date Securities) , mwishoni mwa semina hiyo leo Februari 9, 2018.
Baadhi ya washiriki wakifurahia hotuba ya mgeni rasmi.
Bw. Abdueli Elinaza akitoa hotuba kwa niaba ya washiriki wa semina hiyo.
Meneja Msaidizi, Dawati la Kutatua Malalamiko ya wateja wa mabenki na taasisi za fedha, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT) Bw.Ganga Ben Mlipano, akitambulishwa kwa wana semina kabla ya kuwasilisha mada ya mafanikio na changamoto za dawati hilo.
Meneja Msaidizi, Dawati la Kutatua Malalamiko ya wateja wa mabenki na taasisi za fedha, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT) Bw.Ganga Ben Mlipano, akiwasilisha mada kuhusu mafanikio na changamoto za dawati la kutatua malalamiko ya wateja wa benki na taasisi za fedha.
Bw. Ganga akibadilishana maewazo na Bi.Vicky Msina, kabla ya kuwasilisha mada yake.
Mgeni rasmi, B. Leticia Rweyemamu, (kulia), akiongozana na Bibi.Leah Mzundu, Meneja Idara ya
Uendeshaji Tawila BoT Mtwara, wakati akiwasili ukumbini kufunga semina.
Kutoka kushoto, Bi. Vicky Msina, Bi. Leticia Rweyemamu na Dkt. Suleiman Missango.
No comments:
Post a Comment