Advertisements

Monday, February 19, 2018

KAMALA CUP 2018: BAKOBA 0 v 2 KAHORORO, JUMA BAEZWA NA JORDAN WAFUNGUA LIGI KWA MABAO.


Na Faustine Ruta, Bukoba
Ligi ya mpira wa Miguu "Kamala Cup 2018" imefunguliwa leo Mjini Bukoba kwenye Uwanja wa Kaitaba na kushuhudia Timu ya Bakoba ikichapwa bao 2-0 na Timu ya Kahororo. Bao la kwanza la Timu ya Kahororo Fc lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 80 na Juma Baezwa baada ya kuwachomoka walinzi wa Timu ya Bakoba. Bao la pili lilifungwa dakika ya 83 na Jordan John na mtanange kumalizika kwa 2-0 dhidi ya wenyeji Baokoba Fc. 



Mdhamini wa Ligi hii Mh. Diwani Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo ameipongeza timu hiyo kwa kuanza Ligi hiyo kwa ushindi pia amewataka Wananchi kuendelea kujitolea kuja kuzishabikia Timu za Kata zao na pia akiwashukuru kwa kujitokeza kwa Wingi kama walivyoingia leo kwenye Uzinduzi. Ligi hii ilikuwa ianze siku ya Alhamisi lakini ilisogezwa mbele kutokana na michezo ya Ligi kuu Vodacom inayeondelea hivi sasa. Mdhamini ametaja zawadi za Washindi katika Ligi hiyo kuwa wa kwanza atazawadiwa kitita cha Tsh. Milioni mbili(2) na Mshindi wa Tatu atapatiwa kitita cha Milioni 1 na nusu huku mshindi wa tatu akijinyakulia kiasi cha milioni moja. Ligi itaendelea tena kesho tarehe 19/02/2018 na kuzikutanisha Timu ya Vetran Bkb vs Ijuganyondo na Bilele vs Rwamishenye.

Katika Uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Mnec wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mh. Mutabuzi(kulia). Hapa akiambatana na mdhamini wa Ligi hiyo Diwani Mh. Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo kwenda kusalimia Timu zote mbili muda mfupi kabla ya mtanange kuanza.

Bw. Cletus akiteta Jambo na Mgeni rasmi Mh. Mutabuzi leo kwenye Ufunguzi wa Kamala Cup 2018.
Wadau wa Soka mbalimbali wakifuatilia kwa karibu Ufunguzi huo ulioanza kwa kishindo hii leo kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani mbalimbali na wa vyama tofauti tofauti wamejitokeza kwa wingi katika Ufunguzi huo na kumpa sapoti ya Nguvu Diwani mwezao katika Ufunguzi huo wa Ligi ya mpira wa Miguu. Pia Mgeni rasmi amesema yeye atatoa kiasi cha shilingi Milioni moja kama sapoti yake katika Ligi hiyo.Mgeni Rasmi Mh. Mutabuzi akitoa neno wakati wa Uzinduzi huo.
Msimamizi na mratibu wa Ligi hiyo ya Kamala Ndg Malik Tibabimale a.k.a (Kadunguda) akitoa maelekezo machache katika Uzinduzi huo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.

Mgeni rasmi akisalimiana na Waamuzi wa Mtanange huo ambao ufunguzi wake umefanyika leo hii na kuhudhuliwa na Mamia ya Mashabiki kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.Kikosi cha Timu ya Bakoba Fc kilichoanza dhidi ya Timu ya Kahororo Fc leo hii kwenye Ufunguzi wa Ligi ya Kamala.Kikosi cha timu ya Kahororo Fc kilichoanza kupambana na Timu ya Bakoba Fc leo hii.Mchezaji wa Timu ya Kahororo Fc Erick Edson(Zenden) akimiliki mpira.Mchezaji wa Kahororo Fc jezi naba 10 Jordan John akimtoka mchezaji wa Bakoba. Kipindi cha kwanza Timu zote mbili hakuna laiyeliona lango la mwenzake zilienda mapumziko zikiwa 0-0.
Wakati wa Mapumziko Ngoma ilipamba Moto.

Mdhamini wa Ligi hii Mh. Diwani Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo akiwatuza Wacheza Ngoma.Mdhamini wa Ligi hii Mh. Diwani Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo nae alipata muda akashiriki Ngoma hiyo pendwa ya Kihaya wakati wa Uzinduzi wa Ligi yake na huku mpira ukiwa mapumziko.Dakika chache wakati wa Mapumziko Ngoma iliendelea kuchukua nafasi...Mashabiki wakafurahia Ngoma hiyo!Ngoma ikiwa imeshika kasi!!!
Kipindi cha pili kiliendelea....Kipa wa Bakoba Fc akikimbilia mpira...
Mchezaji wa Kahororo Fc Juma Baezwa akimiliki mpira
Wadau wakitazama mpira
Mdhamini wa Ligi hii Mh. Diwani Kamala Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo akiwa Meza kuu na Mgeni rasmi wakiutazama mpira wakati wa kipindi cha pili. Timu ya Kahororo Fc imeibuka Bingwa kwa bao 2-0 dhidi ya Timu ya Bakoba Fc.
Mashabiki waliingia kwa Wingi katika Uwanja huo wa Kaitaba wakati wa Ufunguzi wa Kamala Cup 2018
Dakika ya 80 Juma Baezwa akipongezwa na wenzake mara baada ya kufunga bao.Kipa wa Kahororo ( kulia) nae alisogea kumpongeza mfungaji.
Matangazaji wa Radio  Kasibante 88.5 Fm  Slay akiteta jambo na Shabiki wa Timu ya Kashai wakati wa Uzinduzi wa Ligi hiyo iliyoana leo.
Bao la pili lilifungwa na Jordan John dakika ya 83 na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya Timu ya Bakoba Fc.
Raha ya bao...
2-0
Kulia kiongozi wa Timu ya Kahororo nae alisogea kuwapongeza Wachezaji wake kwa kuanza kwenye Ligi hiyo huku dakika zikiwa zimeyoyoma.
 Mpaka dakika 90 zinakamilika Bakoba Fc 0 Kahororo 2.

No comments: