ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 28, 2018

MAAFISA ELIMU KUWENI WABUNIFU NA KUONGEZA WELEDI KAZINI-JAFO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara mjini Dodoma leo
Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Zainab Chaula akieleza na kufafanua masuala ya Lishe, Uwajibikaji katika kazi na Utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala kwamba kila mmoja ana jukumu la msingi katika kutekeleza majukumu yake na kutoa huduma bora kwa Watanzania, kabla ya ufunguzi wa kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara mjini Dodoma leo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi Viongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora na Ofisi ya Rais TAMISEMI, pia baadhi ya washiriki wa kikao kazi
cha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara (waliosimama).
Pichani Baadhi ya Washiriki wa kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu,Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara na Wakurugenzi wa Wizara ya Utumishi na Utawala Bora, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI kinachofanyika mjini Dodoma kuanzia tarehe 27 hadi
28 Februari, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe (kulia) akisikiliza jambo toka kwa Naibu Katibu Mkuu OR TAMISEMI (ELIMU), Tixon Nzunda wakati
wa ufunguzi wa kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara mjini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo, amewataka Maofisa Elimu nchini kote kuwa wabunifu kwa kuwapa motisha walimu katika maeneo yao ili wafanye kazi kwa weledi.

Jafo aliyasema hayo alipokua akifungua kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala wasaidizi wa Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara.

Alisema kila Afisa Elimu aoneshe uthubutu na ajipime utendaji kazi wake hali wakiangalia changamoto katika maeneo yao na kutoa taarifa mapema ili ziweze kutatuliwa.

Alisema kwa mfano mkoa wa Dodoma bado una shida ya elimu kwani bado haufanyi vizuri, hivyo Maafisa Elimu wachunguze na kujua tatizo ni nini.

Aidha, alisema Maafisa Elimu wafanye utafiti kubaini changamoto na kutafutia majibu na Ofisi yake ipo tayari kushirikiaana nao ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote watakaofanya vibaya katika sekta hiyo nuhimu.

“Tamisemi ipo tayari kuwasaidi, ila hatutavumilia kama mtafanya vibaya, jukumu lenu kubwa ni kufuata miongozo na kutoa taarifa kwa Viongozi kwani bila kufanya hivyo mtaleta mikanganyiko katika jamii,”alisema

Pia Mhe. Jafo, aliongelea suala la michezo kuwa serikali imeamua kuimarisha michezo katika ngazi zote, kwani michezo na elimu vinaenda sambamba. Watoto wasioshiriki michezo mienendo yao inakua ipo chini hivyo amewaagiza ushiriki wa michezo mashuleni.

Amewaagiza maafisa elimu wasichague wanafunzi ambao sio wawakilishi sahihi wafuate utaratibu wa kuchagua wachezaji kutoka shule zote.

Aliwaagiza Maafisa Elimu wajenge utaratibu wa kujenga uzalendo kwa wanafunzi, wasisitize kuimba nyimbo za kitaifa ili kujenga uzalendo katika nchini.

Katika hatua nyingine, Jafo amewataka Maafisa Elimu kusimamia suala la mazingira mashuleni ili kuunga mkono Kampeni ya Mhe. Makamu wa Rais ya upandaji miti na kusaidia suala zima la kutunza mazingira.

Amewaasa Washiriki hao kubadili Sekta ya Elimu kwa kuboresha ufaulu hadi kufikia asilimia 80 kama sehemu ya majukumu yao.

Naye, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mussa Iyombe aliwataka maofisa hao kuanzia ngazi ya kata hadi mikoa kuacha kuwatesa walimu kwa kuwa wanasababisha wajazane kwenye wizara hiyo kuonana na viongozi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Lauren Ndumbaro aliwasisitiza Maafisa Elimu hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma pamoja na maadili ya taaaluma zao kwani kumekua na malalamiko mengi juu ya ukandamizwaji wa waalimu nchini.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu, amesema kuwabaadhi ya Maafisa Elimu wanashirikiana na baadhi ya walimu kuhujumu vifaa vya maabara mashuleni na kuvipeleka kwenye mashule yao binafsi na kwamba waache tabia hiyo kwani Serikali haitowavumilia.

Dkt. Semakafu amesema Maafisa Elimu waache uonezi kwa walimu pindi wanapotaka kujiendeleza kielimu kwa kuwanyima fursa hiyo kwa kuwasimamishia mishahara yao bila sababu za msingi.

Awali kabla ya ufunguzi wa kikao kazi hicho, Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Zainab Chaula alielezea na kufafanua namna ya kuboresha masuala ya Lishe katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Uwajibikaji katika kazi kwa washiriki na Utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala (CCM) kwamba kila mmoja ana jukumu la msingi kwa mujibu wa Ilani hiyo, katika kutekeleza majukumu yake na kutoa huduma bora kwa Watanzania na hivyo ni wajibu wa kila mshiriki kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na uadilifu kwa maendeleo ya Watanzania.

No comments: