ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 12, 2018

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MRADI WA KUENDELEZA UTALII UKANDA WA KUSINI (REGROW)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla kabrasha lenye Andiko la mradi wa REGROW na Mikataba ya Fedha na utekelezaji wa mradi mara baada ya kuuzindua mradi huo katika eneo la Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) ,Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa uwekezaji katika miundo mbinu ya mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua mradi wa REGROW. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imedhamiria kuleta mabadiliko ya dhati katika sekta ya utalii kwa kuhakikisha inatanua mtandao wa barabara na pia kuweka mikakati dhabiti ya kuviendeleza vivutio vya utalii viliovyoko kanda ya Kusini ili vichangie ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi. 


Makamu wa Rais aliyasema hayo leo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii kanda ya kusini mwa Tanzania uliofanyika Kihesa Kilolo mkoani Iringa.Makamu wa Rais alisema Serikali imeendelea kuandaa na kutekeleza mipango mikakati mabali mbali kwa lengo la kuhakikisha shughuli za utalii zinasambaa nchi nzima .

Makamu wa Rais amasema katika kuendeleza utalii kanda ya kusini, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo mwenye masharti nafuu Dola za kimarekani milioni 150 kutoka benki ya Dunia ambapo mradi huo utatekelezwa kwa miaka 6 kuanzia 2017/2018.

Mradi huo wenye lengo kuu la kukuza utalii na kipato kwa wananchi kwa kuboresha miundo mbinu, kujenga uwezo katika usimamizi wa maliasili na kuwawezesha wananchi wanaozunguka hifadhi kuzalisha kwa tija

“Kama nilivyosema hapo awali mradi huu utajulikana kama Resilient Natural Resource for Tourism and Growth (REGROW) na utaanza kutekelezwa katika maeneo ya hifadhi ya Taifa za Ruaha, Mikumi, Udzungwa na Pori la Akiba Selous “

Makamu wa Rais ameiagiza Baraza la Mazingira lililokuwa chini ya Ofisi yake kuharakisha tathmini ya mazingira ya bonde la mto ruaha mkuu ili kuhakikisha kuwa mradi huu unatekelezwa kwa ufanisi bila athari zozote baadaye za mazingira.

Makamu wa Rais alielekeza taasisi zote zinazohusika zikiwemo Sekretarieti za mikoa, Halmashauri za Wilaya na Vijiji kutoa ushirikiano wa kutosha wa kufanikisha utekelezaji wa shughuli za mradi.“Tuhakikishe sheria zinafuatwa na hakuna uvamizi wala shughuli za binadamu kwenye vyanzo vya maji na hifadhi. Wahenga wanasema tunza mazingira yako yakutunze”.

Makamu wa Rais aliwashukuru benki ya Dunia kwa kukubali kukopesha mkopo wenye masharti nafuu .Aidha kabla ya Makamu wa Rais kuzungumza, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla alisema Sekta ya Utalii ni moja ya sekta za kipaumbele katika uchumi wa Tanzania ambapo takribani asilia 20 ya pato la Taifa linatokana na utalii na robo ya fedha za kigeni zinatokana na Utalii.

No comments: