Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua jengo la ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Itilima.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia watumishi mbalimbali na wanafunzi waliohitimu katika chuo kikuu huria mkoani Simiyu juu ya umuhimu wa elimu ya juu katika ufanikishaji wa viwanda.
Na Shushu Joel,Bariadi.
Vyuo vikuu nchini vimeshauri kuwa chachu ya ufanikishaji wa dhima ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Joseph Magufuli kuhusu mwelekeo wa uchumi wa viwanda nchini.
Hayo yamesemwa jana na Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassani alipokuwa akizindua kongamano la elimu ya juu na Tanzania ya viwanda katika wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
Alisema kuwa ili serikali iliweze kufikia malengo yake inahitaji kuwa na wasomi wengi wenye elimu za juu ambao wataisaidia nchi yao katika ufanikishaji wa dhima ya viwanda kutokana na elimu ya uhakika waliyoipata kutoka vyuoni.
“Wakufunzi wetu wa vyuo mbalimbali nchini wanapowaandaa vijana wetu katika masomo yao basi iwe pia ni chachu ya ufanikishaji wa maendeleo kwa taifa kutokana na kile wanachokipata kutoka kwenye vyuo vyao”Alisema.
Aliongeza kuwa wanachuo kote nchini waondokane na dhana ya kuitegemea serikali katika upataji wa ajira bali wajikite katika kujiajiri ili nao waweze kuwaajiri watanzania wenzao na serikali ipo tayari katika kuwasaidia wale wote wenye nia ya kuanzisha viwanda kwa kuwasaidia katika masoko na vitu vingine.
Aidha mama Samia alitumia muda huo kukipongeza chuo kikuu huria nchini kwa kutawanya elimu karibia kote nchini ili watanzania waweze kujiendeleza kieleimu na si kubaki na elimu waliyonayo tu.
Naye mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amempongeza makamu wa Rais kwa kitendo chake cha kujumuika na watu mbalimbali waliofika katika kongamano hilo lenye kulenga ufanikishaji wa viwanda kupitia elimu ya juu.
Mkuu huyo wa mkoa aliongeza kuwa ili taifa letu lifanikiwe ni lazima watanzania tukasome na hii ni moja ya sababu ya kongamano hilo kufanyika Simiyu ili wana Simiyu waweze kutambua umuhimu wa elimu katika maendeleo.
Aidha mkuu huyo wa mkoa amewataka wakurugenzi katika mkoa wake kutowabania watumishi wote wanaohitaji kuendelea kimasomo kupitia chuo kikuu hulia kilichopo katika mkoa huo.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Huria nchini Profesa Elifasi Bisanda amemuhakikishia Makamu wa Rais kuwa chuo kikuu huria kitahakikisha kinaisaidia serikali katika dhima yake ya viwanda kwa kuzalisha vijana wenye kutambua umuhimu wa kujiajiri kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo.
No comments:
Post a Comment