Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kufanya kikao na Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Nassibu Abdul (Diamond) kujadili namna ya kuboresha maadili katika kazi za sanaa na baadaye kukutana na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza na Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa kikao na waandishi wa habari baada ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) kufanya mazungumzo na Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Nassibu Abdul (Diamond) kujadili namna ya kuboresha maadili katika kazi za sanaa na baadaye kukutana na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa bongo fleva Nassibu Abdul (katikati) akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari baada ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) kufanya naye mazungumzo kujadili namna ya kuboresha maadili katika kazi za sanaa na baadaye kukutana na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtendaji Mkuu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati mwenye miwani) katika picha ya pamoja na uongozi wa WCB baada ya kufanya nao mazungumzo kujadili namna ya kuboresha maadili katika kazi za sanaa na baadaye kukutana na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM
Na: Genofeva Matemu - WHUSM
Watendaji wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo katika sekta ya Sanaa pamoja na Taasisi zake ikiwemo BASATA, Bodi ya Filamu na TCRA wametakiwa kukutana na makundi ya wasanii wa mziki nchini kwa lengo la kuelimisha taratibu za kuwasiliana na mamlaka husika za sanaa ili zijiridhishe na maudhui ya kazi za sanaa kabla ya kuzisambaza.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kufanya kikao na msani wa muziki wa bongo fleva Nassibu Abdul (Diamond) kujadili namna ya kuboresha maadili katika kazi za sanaa na baadaye kukutana na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mwakyembe amesema kuwa maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo yamefanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa kiongozi wa wizara, hivyo wasanii na jamii kwa pamoja waelewe kwamba hatua zilizochukuliwa na Naibu Waziri Shonza hivi karibuni zilikuwa za Wizara kwa mujibu wa sheria za nchi.
“Serikali haina ugomvi wowote na wanasanaa nchini bali ina tatizo na mmomonyoko wa maadili ya kitanzania nchini na kwamba kila mwanasanaa ana wajibu wa kulinda maadili ambayo ni sehemu ya utamaduni wetu” amesema Mhe. Mwakyembe
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amewasisitizia wanasanaa kufuata taratibu za kuwasilisha kazi zao za sanaa mapema kwenye mamlaka husika ili kuepusha matatizo baadaye kwani suala la kulinda maadili ni endelevu.
“Wakati umefika sasa kwa Bodi ya Filamu Tanzania na TCRA kukamilisha zoezi la kuoanisha kanuni za madaraja ya kazi za sanaa ili kazi zinazofaa kuonekana na watu wazima peke yake zianze kuangaliwa saa sita usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi” amesema Mhe. Shonza
Naye msanii wa muziki wa Bongo Fleva Nassibu Abdul (Diamond) ameahidi kushirikiana kwa karibu na Naibu Waziri Shonza na uongozi mzima wa Wizara ya Habari katika kusimamia maadili ya kazi za sanaa na kuwa mfano bora wa wasanii nchini katika kulinda utamaduni wa mtanzania.



No comments:
Post a Comment