Advertisements

Thursday, May 17, 2018

Mbunge Chadema augua ghafla, kesi inayomkabili Yapigwa Kalenda

Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro imeahirisha kesi ya tuhuma za kuchoma ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Sofi baada ya mshtakiwa wa kwanza, Suzan Kiwanga kuugua ghafla.

Kabla ya kuhairishwa kwa kesi hiyo leo Alhamisi Mei 17, 2018, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali,  Sunday Hyera ulionekana kutokubaliana na taarifa hizo za ugonjwa.

Hali hiyo ilimfanya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Ivan Msack kumtaka mdhamini pamoja na wakili wa upande wa utetezi, Barthelomew Tarimo kuwasilisha taarifa ya daktari itakayothibitisha taarifa hizo za ugonjwa.


Wakili Tarimo na mdhamini wa Kiwanga walitoka na kwenda kuchukua taarifa hiyo ya daktari wa kituo cha afya cha Aga khan iliyoeleza kuwa Kiwanga anasumbuliwa na kichwa na maumivu ya mwili na kuiwasilisha mahakamani.

Katika taarifa hiyo ya daktari ilieleza kuwa Kiwanga amepumzishwa kwa saa sita na hivyo Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Mei 18 mwaka huu.

No comments: