Advertisements

Sunday, May 6, 2018

WAZIRI UMMY MWALIMU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KIWANDA CHA DAWA CHA M-PHARMACEUTICALS WILAYANI BAGAMOYO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wapili kulia), akishirikiana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (watatu kulia) Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wanne kulia) na Mwnyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi (watano kulia) wakifunua kitambaa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la kiwanda cha dawa za binadamu unaoatarajiwa kuanza hivi karibuni, ikiwa ni katika juhudi za ukuzaji sekta ya viwanda nchini. Kiwanda hicho kitamilikiwa na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi. Hafla hiyo imefanyika wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (watatu kulia), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wapili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo(wakwanza kulia), Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi(wanne kulia) na viongozi wengine wakimsikiliza Mtaalamu wa michoro, Ruchir Sharma akielezea na kuonyesha ramani ya kiwanda cha dawa kinachotarajiwa kujengwa eneo la Kerege, wilayani Bagamoyo baada ya Waziri Ummy kuweka jiwe la msingi wa ujenzi huo. Hafla hiyo imefanyika wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa Sherehe ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Dawa za Binadamu kinachomilikiwa na Dk. Reginald Mengi, kilichopo Kerege Wilayani Bagamoyo, ambapo aliwahakikishia wawekezaji wazawa katika sekta ya afya kupata ushirikiano kutoka serikalini.Hafla hiyo imefanyika wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza wakati wa Sherehe ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Dawa za Binadamu kinachomilikiwa na Dk. Reginald Mengi, kilichopo Kerege Wilayani Bagamoyo, ambapo aliwahakikishia wawekezaji wazawa katika sekta ya viwanda na uwekezaji kupata ushirikiano kutoka serikalini.Hafla hiyo imefanyika wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi, akizungumza wakati wa Sherehe ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Dawa za Binadamu kilichopo Kerege Wilayani Bagamoyo, ambapo alishukuru ushirikiano aliopata kutoka serikalini wakati wa mchakato wa uanzishwaji kiwanda hicho .Hafla hiyo imefanyika wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.
Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka kulia ni Mkuu wa Gereza la Bagamoyo,Muyengi Machumu,Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Magereza,Malisa Emmanuel na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bagamoyo Adam Maro, wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(hayupo pichani) wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha dawa za binadamu Kerege wilayani Bagamoyo.



Wasanii kutoka Chuo cha Sanaa Bagamoyo wakitoa burudani wakati wa Sherehe za Uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha dawa za binadamu unaoatajiwa kuanza hivi karibuni katika eneo la Kerege, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. (PICHA NA ABUBAKARI AKIDA)

No comments: