Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa akitoa salamu za Wilaya jana mara baada ya Wajumbe wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa sasa na baadhi ya waliomaliza muda wao kutembelea Wilaya hiyo kwa ajili ya makabidhiano na kutembelea wanufaika.
Mratibu wa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Seraphia Mgembe akitoa ufafanua jana kwa wamefanikiwa urasimishaji wilayani Urambo wakati Wajumbe wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa sasa na baadhi ya waliomaliza muda wao walipowatembelea.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) aliyemaliza muda wake Captian Mstaafu John Chiligati akitoa ufafanua jana kwa wamefanikiwa urasimishaji wilayani Urambo wakati Wajumbe wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa sasa na baadhi ya waliomaliza muda wao walipowatembelea.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Balozi mstaafu Daniel ole Njoolay akitoa ufafanua jana kwa wamefanikiwa urasimishaji wilayani Urambo wakati Wajumbe wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa sasa na baadhi ya waliomaliza muda wao walipowatembelea. Picha na Tiganya Vincent.
Na Tiganya Vincent, Tabora
HALMASHAURI ya Wilaya hapa nchini zimetakiwa kutenga maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo wa shughuli mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidisa kukopesheka na asasi za kifedha.
Ombi limetolewa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).aliyemaliza muda wake Captain Mstaafu John Chiligati wakati akiongea na uongozi wa Wilaya na ule Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Alisema uongozi wa Halmashauri umekuwa ukitumia fedha nyingi zake katika kuwalipa posho Mgambo ambao wamekuwa wakifukuza wafanyabiashara wadogo wadogo wakiwakuta wamepanga biashara katika maeneo ambayo sio rasmi badala ya kutumia fedha hizo kwa ajili ya kutenga eneo ambalo watawekwa pamoja ili kuendesha shughuli zao.
“Nawaomba Halmashauri tengeni maeneo ambayo mtawapanga wafanyabiashara kulingana na shughuli zao …kama ni mvua nguo mtaweka sehemu Fulani…kama anauza viatu atakuwa eneo lake ili kuwafanya watu wa Benki iwe kwao rahisi kuwakopesha…benki haziwezi kukopesha mtu anayetembeza bidhaa”alisema.
Aidha aliomba Serikali kuongeza idadi ya Maofisa Biashara katika Halmashauri ili waondoke Maofisini na kwenda kuwasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo jinsi ya kuboresha biashara zao na kuongeza kuwa hivi sasa idadi yao ni ndogo na hivyo kushindwa kuwasaidia wananchi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya MKURABITA Balozi mstaafu Daniel ole Njoolay alizitaka Halmashauri zote hapa nchini kuhakikisha zinashirikiana na wadau wengine kuwasidia wananchi kugeuza ardhi , biashara na mali zao nyingine kuwa mitaji hai na sio mfu ili waweze kupiga hatua.
Alisema uhai wa rasilimali zao kama vile ardhi na biashara ndio zitawapa nguvu ya kwenda katia Benki kwa ajili ya kukopa kwa ili kupanua biashara zao.
Balozi Njoolay alisema bila watu kukopa hawataweza kupanua na kuimarisha biashara zao.
Kwa upande wa Mratibu wa MKURABITA Seraphia Mgembe alisema wamefanikiwa kurasimisha ardhi ya Vijijini katika Halmashauri 50 za Tanzania bara, 4 za Zanziabar na kwa upande wa ardhi ya mijini wamerasimisha katika Halmashauri 12 na biashara katika Halmashauri 10.
No comments:
Post a Comment