Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la Kituo cha Afya cha Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi waTunduma kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake mkoani Songwe.
Sehemu ya Umati wa wakazi wa Tunduma waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Tunduma mara baada ya kukifungua ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Esther Luila mwenye umri wa miaka 7 mara baada ya kukifungua kituo cha Afya Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na Wajasiriamali wa Wilaya ya Momba muda mfupi kabla hajahurubia kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Utawala Bora ni moja ya ahadi waliyoitoa kwa wananchi wakati wa kampeni.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika mkoa wa Songwe.
“Lazima tunapofanya kazi zetu sheria zifuatwe, unapoacha kufuata sheria kwa sababu ya Matakwa binafsi, kwa sababu ya kunufaika wewe binafsi hili ni Tatizo hapa hapana utawala bora”
alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais alisema Utawala bora usisukumwe tu upande wa Serikali unapaswa kupimwa kwenye ngazi zote mpaka za chini zikiwemo ngazi za Udiwani.
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Utawala bora ni pamoja na maendeleo ya Serikali yanapatikana.
Makamu wa Rais amesema Serikali itajenga pamoja na kuboresha vituo vya Afya 9 katika mkoa wa Songwe ambapo wilaya ya Momba kutakuwa na vituo vitatu.
Mapema leo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefungua kituo cha Afya cha Tunduma kilichofanyiwa maboresho na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 500 na ambacho kitahudumia wakazi zaidi ya elfu 80.
“Naomba sana Wananchi wa Tunduma pimeni Afya zenu, Serikali imetumia pesa nyingi kuweka mashine pale, kuweka mambo yote ambayo yanapaswa katika kutumika katiuka kupima afya, na naposema kupima afya simaanishi maradhi ya ukimwi peke yake lakini mashine zile zina pima mambo mengi” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amesema upatikanaji wa Dawa ndani ya mkoa wa Songwe umekuwa kwa kiasi kikubwa.
Makamu wa Rais ameutaka Uongozi wa mkoa kuwasaidia kuwaendeleza vijana wajasiriamali ambao ni wabunifu na kuwasaidia kupata mikopo ya masharti nafuu.
No comments:
Post a Comment