Advertisements

Friday, July 13, 2018

TAZAMA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018 HAPA

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde

BARAZA la Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza matokeo ya kidato cha sita leo Julai 13 na kuzitaja shule zilizoshika mkia kuwa ni pamoja na ya wasichana ya Jangwani, ya Jijini Dar es Salaam.

Ubora wa ufaulu kwa watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 72,866 sawa na 95.52% wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu wakiwemo wasichana 30,619 sawa na 95.92% na wavulana 42,247 sawa na 95.23%. Waliopata daraja la kwanza ni 8,168.

No comments: