Muuguzi Mkuu wa Hospitali Teule ya Rubya iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Sister Theonestina John, akimsaidia Sajida Said (36) mkazi wa Kijiji cha Lubao Kata ya Ijumbi, aliyejifungua watoto watatu mapacha katika hospitali hiyo jana.
Sajida Said (36), akiwa na mapacha wake hao.
Na Dotto Mwaibale, Muleba Kagera
MKAZI wa Kijiji Lubao kilichopo Kata ya Ijumbi Wilayani Muleba mkoani Kagera, Sajida Saidi, amejifungua watoto mapacha wenye afya njema katika Hospitali Teule ya Rubya iliyopo Muleba mkoani Kagera.
Akizungumza na waandishi wa habari wilayani humo leo hii, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt.George Kasibante alisema hali ya mama huyo na watoto wake aliojifungua juzi ni nzuri.
"Watoto hawa waliozaliwa kabla ya muda wao wanaendelea vizuri na sasa wapo kwenye wodi maalumu ya joto" alisema Kasibante.
Alisema katika Hospitali hiyi ili ni tukio la pili kwa mama kujifungua watoto mapacha zaidi ya wawili kwani mwaka jana kuna mama mwingine alijifungua watoto watatu.
Alisema uzito wa watoto hao umetofautiana kwani yupo mtoto wa kilogramu 2.1, 2.1 na 2.6.
Mama wa watoto hao Sajida mwenye wa watoto watano ambapo sasa atakuwa nao nane amesema anajisikia vizuri kupata watoto hao ukizingatia naye kuwa alizaliwa pacha na mwenzake aitwaye Shakira Saidi.
No comments:
Post a Comment