ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 12, 2018

RAIS DKT MAGUFULI ATEKELEZA AHADI YAKE KWA KUKABIDHI MATREKTA 10 KWA CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE (SUA) CHA MOROGORO

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibunda wapili kutoka (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa NDC Profesa Damian Gabagambi wakwanza (kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo wapili kutoka (kulia), akikata utepe kuzindua Matrekta 10 ambayo ameyakabidhi kwa Chuo hicho cha SUA kutekeleza ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipotembelea chuo hicho mkoani Morogoro tarehe 7 Mei 2018.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akipunga mkono pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuzindua na kuyakabidhi Matrekta hayo 10 kwa Chuo cha SUA katika hafla fupi iliyofanyika katika kiwanda cha kuunganisha Matrekta hayo cha URSUS- TAMCO Kibaha mkoani Pwani.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akiangalia ubora wa  moja ya matrekta hayo 10 aliyoyakabidhi kwa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA.

 Sehemu ya Matrekta 10 yaliyokabidhiwa kwa Chuo cha SUA ikiwa ni  utekelezwaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipotembelea chuo hicho mkoani Morogoro tarehe 7 Mei 2018.
 Sehemu ya Matrekta 10 yaliyokabidhiwa kwa Chuo cha SUA ikiwa ni  utekelezwaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipotembelea chuo hicho mkoani Morogoro tarehe 7 Mei 2018.

 Sehemu ya Matrekta 10 yaliyokabidhiwa kwa Chuo cha SUA ikiwa ni  utekelezwaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipotembelea chuo hicho mkoani Morogoro tarehe 7 Mei 2018.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akizungumza katika hafla hiyo fupi ya kukabidhi ya matrekta 10 aliyoyakabidhi kwa Chuo cha Kilimo cha Sokoine SUA katika kiwanda cha kuunganisha Matrekta cha URSUS- TAMCO Kibaha mkoani Pwani.
PICHA NA MPIGA PICHA WETU

Na Sultani Kipingo, Kibaha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kutoa matrekta 10 kwa Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ili kuimarisha utoaji wa mafunzo ya kilimo na kuzalisha wataalamu bora wa kilimo nchini.
Matrekta hayo 10 aina ya Ursus yamekabidhiwa Jumamosi Agosti 11, 2018 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James huko Kibaha Mkoani Pwani na kueleza kuwa SUA imepatiwa matrekta hayo ikiwa ni juhudi za Serikali za kuendeleza kilimo ambacho kinatoa ajira kwa watanzania wengi.
Matrekta hayo yana thamani ya Shilingi Milioni 587.5
Bw. Doto James amekitaka Chuo Kikuu cha SUA kuyatumia matrekta hayo vizuri na kwamba Serikali itafuatilia kupitia kitengo cha Wizara ya Fedha na Mipango cha kufuatilia fedha za miradi ya maendeleo katika taasisi ambayo inapokea fedha za Serikali.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SUA Prof. Yonika Ngaga amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi hiyo pamoja na kutekeleza ahadi ya kujenga mabweni ya chuo, ambapo SUA imepokea shilingi Bilioni mbili na kuahidi kuwa chuo kitajiimarisha zaidi katika utoaji taaluma bora ya kilimo inayoendana na wakati wa sasa.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Mandeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Japhet Justine amesema benki hiyo imejipanga kumuondoa mkulima katika kilimo cha jembe la mkono na kumpeleka katika kilimo cha kisasa na kinachotumia zana za kisasa, hivyo ametoa wito kwa wakulima kutumia benki hiyo kupata mikopo itakayowasaidia kulima kisasa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Prof. Damiani Gabagambi amesema Tanzania ina mahitaji ya matrekta milioni 6 ikilinganishwa na matreka takribani 30,000 yaliyopo na hivyo ametoa wito kwa wakulima na wadau wa kilimo kujitokeza kununua matrekta mengi zaidi ili yatumike kulima katika eneo kubwa linalofaa kwa kilimo hapa nchini.
Akiwa ziarani mkoani Morogoro Mhe. Rais Magufuli alitembelea Chuo Kikuu cha SUA na kujulishwa kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba na ubovu mkubwa wa matrekta na ukosefu wa mabweni ya wanafunzi hali iliyokuwa ikiathiri utoaji wa taaluma ya kilimo na hivyo akaahidi kununua matrekta hayo pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni, ahadi ambazo amezitekeleza.

No comments: