Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin William Mkapa akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara tu alipoingia kwenye banda la Magereza kwenye maonesho ya Nane nane yaliyofanyika Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Meneja masoko wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Msaidizi Yunge Saganda(tisheti ya Njano na kofia) akitoa maelezo ya namna bidhaa za ngozi zinavyozalishwa kama moja ya shughuli za urekebishaji wa wafungwa katika Gereza Karanga. Mkono wa kulia wa Yunge ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ndg. Antony Mtaka na nyuma ya Mh. Rais Mstaafu ni Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally.
Mrakibu Msaidizi Yunge Saganda(tisheti ya Njano na kofia) akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa jinsi bidhaa za nafaka zinazolimwa na wafungwa chini ya uangalizi wa Askari Magereza kama njia ya urekebishaji kwa vitendo zinavyopatikana katika Magereza mbalimbali nchini.
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akiangalia meza ya chai(coffee table) iliyotengenezwa kisanii na kunakshiwa vizuri na wafungwa toka Gereza Uyui Tabora kama moja ya njia za urekebishaji wa wafungwa Magerezani.Kushoto kwa Mh. Rais Mkapa, ni Mama Anna Mkapa ambaye aliaambatana na Mh. Rais.
No comments:
Post a Comment