Advertisements

Friday, August 3, 2018

WAZIRI ISACK KAMWELWE AKAGUA KIWANJA CHA NDEGE CHA MOSHI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) mkoa wa Kilimanjaro Bw. Julius Mlungwana (kulia), wakati akikagua Kiwanja cha Ndege cha Moshi, mkoani humo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua barabara ya kuruka na kutua ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) mkoa wa Kilimanjaro Bw. Julius Mlungwana (kulia), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto), hati ya kiwanja cha Ndege cha Moshi wakati alipokuwa akikagua kiwanja hicho, mkoani humo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Prof. Ninatubu Lema, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, wakati akikagua barabara ya kuruka na kutua ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Moshi, mkoani Kilimanjaro.(PICHA NA WUUM)

No comments: