Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa , MNEC Theresia Mtewele aliyeshika Ilani ya chama cha mapinduzi akiwa sambamba na diwani wa kata ya kitwiru Baraka Kimata ,MNEC Mussa Mwakitinya na mkurugenzi wa TAEDO Kenani Kihongosi ambaye pia ni mwenyekiti wa vijana wa ccm mkoa wa Iringa (UVCCM) akielezea jinsi ilani ya CCM inayotekelezwa kwa kutoa elimu mbalimbali ikiwapo elimu ya wajasiliamalia ambayo ilitolewa siku hiyo katika kata ya kitwiru kwa wananchi wote waliojitkeza
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa anayewakilisha vijana, MNEC Theresia Mtewele, amewataka wajasiriamali wa mkoani Iringa kuwa na ubunifu kwenye biashara zao,kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha za kibiashara ili kukuza mitaji yao pamoja na kujiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa mikopo itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza wakati wa ufunguaji wa mafunzo ya ujasirilimali yaliyoratibiwa na Diwani wa Kata ya kitwitu, Baraka Kimata na kutolewa na taasisi ya TAEDO, MNEC Mtewele alisema wajasariliamali wengi wamekuwa hawakopesheki kwa sababu hawajajiunga katika vikundi.
“Ili kuendana na sera ya Serikali ya viwanda wajasiriliamali hawana budi kujiunga katika vikundi vidogo ili kupata mikopo itakayowasaidia kuanzisha viwanda vidogo jambo ambalo litawasaidia kuongeza kipato na ajira kwa watu wengine,” amesema.
MNEC Mtewele aliwataka wajasiriamali wa Iringa kuwa wabunifu katika biashara zao ili kuweza kufanikiwa zaidi
“ili mjasiriliamali aweze kufanikiwa lazima awe na nidhamu na fedha anayopata na si kuitumia hovyo kwani itasababisha kuyumba kwa biashara na hatimaye kufilisika”
Kwa upande wake Diwani Kimatha, alisema aliamua kutoa mafunzo hayo bure kwa wananchi wake ili kujikwamua kiuchumi na kujijengea ajira kuliko kusubiri kuajiriwa.
Kimata alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwakwamua wananchi wake kiuchumi ikiwa pamoja na kuunga mkono jitihada za Mh.Rais John Pombe Magufuli juu ya Tanzania ya viwanda huku akiwashauri viongozi wenzie kutumia nafasi za uongozi kwa kuwasaidia wanaowaongoza.
Nao baadhi ya wananchi wa kata ya kitwiru mkoa wa Iringa wamemshukuru diwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata kwa kuwasaidia kupata mafunzo ya ujasiriamali, huku wakiahidi kuunga mkono sera ya Tanzania ya viwanda kwa kufungua viwanda vidogo vidogo mara baada ya mafunzo hayo .
Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi wa kata ya kitwiru katika semina ya mafunzo ya ujasiriamali inayolenga ufugaji wa kuku na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali , ambapo wamemshukuru diwani wa kata huyo kwa kitendo cha kugharamia mafunzo hayo kwao ,huku wakiahidi kuunga mkono sera ya Tanzania ya viwanda mara baada ya kumaliza mafunzo hayo.

No comments:
Post a Comment