Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Msataafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ,Davis Mwamnyange akiwa ameongozana mwenyeji wake ,Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA,Mhandisi Cyprian Luhemeja alipofanya ziara ya kutembelea Miradi Mikubwa ya Maji katika jiji la Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Msataafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ,Davis Mwamnyange akipanda kwenye moja ya Matanki Makubwa ya kuhifadhia Maji katika eneo la Goba kuangalia maenedeleo ya ujenzi wa tanki hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA,Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuonesha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Msataafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ,Davis Mwamnyange maeneo ambayo yatanufaika na huduma ya maji Safi mara baada ya miradi hiyo kukamilika.
Sehemu ya Matengenezo katika mradi huo ukiendelea.
Moja ya Matanki ya kuhifadhia maji ambalo matengenezo yake yanaendelea.
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA,Mhandisi Cyprian Luhemeja akionesha ramani kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Msataafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ,Davis Mwamnyange ,maeneo ambayo tayari zoezi la upanuzi wa mtandao wa huduma ya maji unfanyika.
Moja ya eneo la Mradi wa kusukm maji ambao ujenzi wake unaendelea.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA,Mhandisi Cyprian Luhemeja akimueleza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Msataafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ,Davis Mwamnyange alipotembelea moja ya mradi unaojengwa kwa ajili ya mashine za kusukuma maji .
Moja ya Transfoma zilizofungwa katika Mashine za kusukuma maji kwa ajili ya kuhakikisha umeme una pozwa kabla ya kuingia kwenye mtambo.
Sehemu ya chini ya tenki ambayo hutumika kwa ajili ya kuhifadhi maji kabla ya kwenda kwa watumiaji .
Tenki kubwa la kuhifadhi maji lilipo katika eneo la Kibamba ambalo tayari limeanza kufanya kazi ka sasa.
Anaandika Dixon
Busagaga,Dar es Salaam .
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na
Majitaka Dar es Salaam na Pwani (DAWASA) Jenerali Mstaafu wa Majeshi ya Ulinzi ,Davis Mwamnyange
amewatoa hofu wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Pwani juu ya upatikanaji wa
huduma ya Maji .
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya
kutembelea miradi mikubwa ya Majisafi kwa
ajili ya kujionea maendeleo ya miradi hiyo ,Jenerali Mwamnyange amesema
kukamilika kwa mradi huo kwa kiasi kikubwa kutapunguza adha ya maji kwa baadhi
ya maeneo kama si kumaliza kabisa tatizo la maji .
Miongoni mwa maneo ya mradi aliyotembelea ni pamoja na mfumo
wa Maji uliopo Bunju,mfumo wa maji Salasala,mfumo wa maji Makongo na
Changanyikeni pamoja na kutembelea
Matanki ya kuhifadhia Maji katika maeneo ya Madale ,Goba na Kibamba.
Jenerali Mwamnyange akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa
kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi ,DAWASA ,Mhandisi Gaudence Aksante
pamoja na mwenyeji wao ,Afisa mtendaji Mkuu wa DAWASA,Mhandisi Cyprian Luhemeja
ameonesha kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huku akiwataka Wakandarasi
kukamilisha miradi hiyo kama walivyokubaliana.
“Ziara hii imekuwa fursa nzuri sana kwangu kama mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA,nimeweza kujionea mwenyewe hali halisi ya mradi
huu itakaoongeza huduma ya Maji katika
jiji la Dar es Salaam “alisema Jenerali Mwamnyange.
“Hatua iliyofikiwa ni nzuri ,inatia moyo na wananchi wawe na
matumaini makubwa kwamba sasa huduma ya maji itakua bora zaidi baada ya
kukamilika kwa mradi huu,Kasi ya Wakandarasi sasa hivi wanajitahidi baada ya
hatua kuchukuliwa na Mamlaka kuwahimiza pamoja na serikali kupitia Wizara ya Maji
na Umwagiliaji”aliongeza Jenerali Mwamnyange .
Alisema licha ya changamoto walizoeleza awali zilizochangia
kupungua kwa kasi ya ujenzi wa mradi huo tayari matatizo yale yametatuliwa na sasa wanaendelea vizuri na kwamba kwa kasi
iliyopo wataweza kumaliza mradi ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.
Kwa upande wake Afusa Mtendaji Mkuu ,Dawasa,Mhandisi Cyprian
Luhemeja alisema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza huduma ya upatikanaji wa
maji ambapo watu Milioni moja wanataraji kufikiwa na huduma.
Alisema mradi huo ukianza hali ya mivujo ya maji iliyopo kwa
baadhi ya maeneo itapungua kwa sababu maji yataenda kwa watu na kwamba awali
tatizo lililokuwepo ni kwamba maji yalikuwa ni mengi lakini mtandao wa maji ni
mdogo kwa sasa matumizi yataongezeka.
“ Tatizo la wizi wa maji nalo pia tunatarajia kuisha ,kwa
sababu wizi wa maji ulikuwepo kutokana na kukosekana kwa maji ,lakini sasa
huduma ya maji ipo na tayari tumeanza kuwananishia wananchi maji kwa mkopo
hivyo wajitokeze tu kuomba kuunganishiwa huduma ya maji.”alisema Mhandisi
Luhemeja.
Mwisho.












No comments:
Post a Comment