Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson (kushoto) na Mwanzilishi mwenza wa Apps & Girls ambao ni waandaaji wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali, Bi. Carolyne Ekyarisiima wakiwasili ndani ya ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa kushiriki jukwaa hilo lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini.
Afisa anayeshughulikia Utamaduni kutoka Ubalozi wa Marekani, Bw. Jeffrey Ladenson akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson (hayupo pichani) kufungua jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson akizungumza na mabinti wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Mwanzilishi mwenza wa Apps & Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima akizungumzia shindano la ubunifu wa programu za kompyuta ambalo limelenga kuhakikisha kwamba binti anawezeshwa katika ulimwengu wa kidijiti wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Mtaalamu wa Mambo ya Sheria, Bi. Gloria Kasununu akielezea taratibu za kisheria za kusajili biashara au kampuni kwa vijana chini ya miaka 18 wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Mkufunzi wa masuala ya Tehama, Bi. Nguse Ngulumbi akitoa mafunzo kwa vitendo kwa baadhi ya wasichana wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Nancy Kaizilege akifafanua jinsi gani vijana wanavyoweza kubuni miradi inayolenga kufikia malengo ya maendeleo endelevu wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Mwananfunzi wa Shule ya Sekondari Kondo wa kidato cha tatu, Saada Thabit akizungumzia vipaji vilivyojificha mbele ya majaji na washiriki wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Kutoka kushoto ni Ofisa anayeshughulikia mambo ya Umma wa Ubalozi wa Marekani, Bi. Brinille Ellis, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson pamoja na Mwanzilishi mwenza wa Apps & Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima wakifurahia jambo wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
aadhi ya wasichana 156 kutoka shule 25 za Dar es salaam walioshiriki jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson katika picha ya pamoja na wasichana 156 kutoka shule 25 za Dar es salaam wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Baadhi ya wanafunzi wakihamasisha lengo namba 14 la malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Na mwandishi wetu
KAIMU Balozi wa Marekani nchini Dk. Inmi Patterson amewataka mabinti wa Tanzania kufikiria taifa lao na namna ambavyo wanaweza kusaidia kuondoa changamoto mbalimbali zinazokabili jamii yao.
Kauli hiyo ameitoa katika jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali lililoshirikisha mabinti wa sekondari wa mkoa wa Dar es salaam; pamoja na mambo mengine walishiriki katika shindano la ubunifu wa programu za kompyuta.
Jukwaa hilo linalojulikana kama Girls Entrepreneurship Summit (GES) 2018 linachagiza mabinti kutumia Tehama kutatua matatizo yaliyopo katika jamii.
Jukwaa hilo lililoandaliwa na ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini limelenga kusaidia mabinti kuchangia utatuzi wa matatizo kwa kuwa wabunifu katika ujasiriamali.
Kaimu Balozi huyo aliwataka mabinti hao kuwa na uvumilivu katika kukabiliana na changamoto zilizopo na kujenga mtandao ambao utawasaidia kuendelea mbele zaidi kiuchumi.
Alisema mtaji mkubwa wa wajasiriamali ni ubunifu na wazo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi bila kuogopa changamoto zilizopo.
Mapema katika hotuba yake Mwanzilishi mwenza wa Apps &Girls, Carolyne Ekyarisiima alisema kwamba jukwaa hilo na mashindano hayo yamelenga kuhakikisha kwamba binti anawezeshwa katika ulimwengu wa kidijiti kwa kumsogezea vishawishi mbalimbali vinavyompa motisha kuwa mbunifu kwa kutumia tehama.
Ekyarisiima alisema kuna changamoto nyingi katika jamii ambazo zinaweza kutatulika kirahisi kwa kutumia Tehama hivyo ipo haja ya mabinti kutambua suala zima la Tehama na matumizi yake hasa programu husika.
Mwanzilishi huyo alisema ili kuwezesha mafanikio katika mradi huo wameshirikiana na shule mbalimbali kuchagua na kisha kuwapata wanafunzi walioshiriki katika mchakato wa mafunzo na kubuni program za kuwezesha ubunifu kwa njia ya Tehama.
Wabinti hao kutoka sekondari mbalimbali za Dar es salaam walipikwa kwa miezi mine huku wakisaidiana katika makundi kutoa suluhu katika matatizo yanayokumba jamii zinazowazunguka.
Amesema mambo yaliyokuwa yanafanywa yalikuwa yaendana na lengo namba 17 la Umoja wa Mataifa la maendeleo endelevu.
Katika tamasha hilo la siku mbili lililofanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam pia wanafunzi kutoka shule ya Lyra mkoani Iringa walifika kuangalia mfumo wa mashindano ili nao waanze.
Akizungumza manufaa ya mradi huo mmoja wa washiriki Jomitrida Jorum wa kidato cha pili shule ya sekondari Kibasila alishukuru kuwapo kwa shindano hilo kwani yeye na timu yake wametengeneza app ambayo inawezesha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kupitia michezo mbalimbali iliyopo katika app hiyo.
Moja kati ya mafunzo waliyoyapata wasichana kutoka Apps and Girls ni pamoja na program za kompyuta kama vile MTHL, Java, Scratch na Arduino. Hizi ni programu adhimu za kompyuta zinazomuwezesha mwanafunzi kutengeneza tovuti, application za simu pamoja na kutengeneza roboti.
Shirika la Apps and Girls linalenga kuziba pengo lililopo ambapo wasichana na wanawake kwa ujumla wako nyuma katika elimu ya dijiti na sayansi kwa ujumla. Hivyo shirika hilo linatoa elimu ya programu za kompyuta bure kwa watoto wa kike ili kuwawezesha kupata maarifa ya kidijitali na kuondoa pengo lililopo kwa sasa.
No comments:
Post a Comment