ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 10, 2018

UBALOZI WA POLAND WAADHIMISHA MIAKA 100 YA UHURU

Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisoma hotuba katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Taifa ya Poland iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi jijini Dar Es Salaam tarehe 09 Novemba 2018. 
Mhe. Krzysztof Buzalski, Balozi wa Poland nchini akisoma hotuba katika hafla ya kuadhimisha miaka 100 ya uhuru wa Poland 
Baadhi ya wageni mbalimbali walioshiriki hafla hiyo wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za kutimiza miaka 100 ya Uhuru wa Taifa la Poland. Sherehe hizo zilifanyika katika makazi ya Balozi wa Poland, Mhe. Balozi Krzysztof Buzalski yaliyopo Oystberbay, Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Novemba 2018

Katika Sherehe hizo, Naibu katibu Mkuu pamoja na mambo mengine alifafanua kuwa uhusiano baina ya Poland na Tanzania ni wa kihistoria na kuwa unaimarika siku hadi siku. 

Pamoja na kuishukuru Poland kwa uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo, amemuomba Balozi Buzalski, kuongeza jitihada katika kuvutia wawekezaji zaidi wa Poland kuja kuwekeza hapa nchini na kusaidia kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania nchini Poland.

Naibu Katibu Mkuu amemhakikishia Balozi wa Poland kuwa Wizara na Serikali kwa jumla itampa ushirikiano wakati wowote atakapohitaji ili kufanikisha malengo kwa manufaa ya mataifa yote mawili. 

No comments: