ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 5, 2018

Dk Mengi afungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa Kichina

 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi akiwa ameambatana na Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke mara baada ya kuwasili wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi kwa wawakilishi wa makampuni   17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi akiongozana na Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China, Bw. Lyu Xinhua kuelekea kwenye eneo maalum kushiriki hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi kwa wawakilishi wa makampuni   17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi akizungumza wakati wa chakula cha mchana alichowaandalia wawakilishi wa makampuni   17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Bw. Louis Accaro, Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China, Bw. Lyu Xinhua, Balozi wa China nchini  Mhe. Wang Ke, Mkurugenzi Mtendaji wa  IPP Touchmate, Bw. Victor Tesha pamoja Msaidizi wa Dk. Mengi, Bw. Godfrey Bitesigirwe.

 Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China, Bw. Lyu Xinhua kutoa salamu wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi kwa wawakilishi wa makampuni   17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa  IPP Touchmate, Bw. Victor Tesha (wa pili kulia) pamoja Msaidizi wa Dk. Mengi, Bw. Godfrey Bitesigirwe (kulia).
 Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China, Bw. Lyu Xinhua akitoa salamu kwa niaba ya ujumbe huo wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi kwa wawakilishi wa makampuni   17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi
 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi akimshukuru Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke kwa kumtambulisha vyema wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi kwa wawakilishi wa makampuni  17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi akipokea zawadi kutoka kwa Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China, Bw. Lyu Xinhua wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi kwa wawakilishi wa makampuni   17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.


Sehemu ya wafanyabiashara wawakilishi wa makampuni  17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji waliposhiriki hafla fupi ya chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China, Bw. Lyu Xinhua pamoja na Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi kwa wawakilishi wa makampuni  17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi akiwa katika picha za kumbukumbu na baadhi ya wafanyabiashara kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi amewaalika wafanyabiashara kutoka China washirikiane naye kuwekeza nchini kwa ubia katika miradi mbalimbali, wakati huu  ambapo Tanzania inapojizatiti kuwa ya viwanda.
Dr Mengi ametoa rai hiyo jijini Dar es salaam wakati wa chakula cha mchana alichowaandalia  wawakilishi wa makampuni   17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji, walioambatana kwenye hafla hiyo na Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke.
Amesema Tanzania ni nchi iliyojaaliwa fursa nyingi za uwekezaji kutokana na utajiri wake wa  raslimali na kusisitiza kuwa waliotayari kushirikiana naye katika miradi mbalimbali kama ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Tanzania hadi Uganda wajitokeze.
Akizungumza katika hafla hiyo Balozi wa China nchini  Mhe. Wang Ke amesema ofisi yake itakuwa kiunganishi  baina ya Wafanyabiashara wa China na Dr Mengi katika kufanikisha pendekezo la kuanzisha kwa ubia hapa nchini viwanda mbalimbali.
Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara hao Bw. Lyu Xinhua amesema amekuja na ujumbe kutoka makampuni 17 ya China yanahusika na shughuli mbalimbali kuanzia ujenzi wa miundombinu, uhandisi, teknolojia ya mawasiliano nk, na kuahidi kuwasilisha mapendekezo yaliyotolewa kwa makampuni husika kwa ajili ya hatua zaidi za utekelezaji.

No comments: