
Mtuhumiwa aliyekamatwa kwa kujifanya afisa kutoka baraza la mitihani(katikati) akiwa chini ya ulizi wa polisi baada ya kukamatwa akiwa katika shule ya Serengeti alipotaka kukagua kwa kufanya vibaya matokeo ya kidato cha nne jana.,Picha na Anthony Mayunga
Serengeti. Maofisa wa Baraza la Mitihani (Necta) wanategemea kutua Serengeti kwa ajili ya kumhoji ofisa feki wa Necta aliyeendesha ukaguzi kwa shule ya Serengeti Nuru.
Ofisa huyo aliyejitambusha kwa majina ya Athumani Salumu, alikamatwa Januari 24 mwaka huu wakati akiendesha ukaguzi katika Shule ya Sekondari Serengeti Nuru ili kujua kwa nini katika mitihani ya kidato cha nne mwaka jana walipata sifuri nyingi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mara, Juma Ndaki ameiambia Mwananchi Digital kwa njia ya simu kuwa baada ya mahojiano ya maofisa hao ndipo watamfikisha mahakamani.
"Tumeshindwa kumfikisha mahakamani baada ya maofisa kutoka Necta kuomba kuja kufanya naye mahojiano ili kupata taarifa mbalimbali za jinsi alivyokuwa akiendesha utapeli wake," amesema.
Soma Zaidi: Bosi ‘feki’ Necta aendesha ukaguzi shuleni, ashtukiwa
No comments:
Post a Comment