Advertisements

Friday, January 11, 2019

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA WANANCHI KUPOKEA NDEGE YA PILI YA AIRBUS A220-300 UWANJA WA NDEGE WA JNIA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria kupokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 iliyowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019
Maafisa waliokwenda Canada kuipokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 wakilakiwa kwa shangwe Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Isaack Kamwelwe wakipewa maelezo na Rubani Patrick kuhusu ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 walipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019.(PICHA NA IKULU)

No comments: