ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 27, 2019

WAZIRI AWATAKA WALIMU WAKUU KUTOA USHIRIKIANO ILI KUANZISHA CLUB ZA VIJANA MASHULENI

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella wakichangia mada wakati wa hafla ya kutimiza miaka 20 ya Shirika la FEMA jana jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella wakichangia mada wakati wa hafla ya kutimiza miaka 20 ya Shirika la FEMA jana jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy pamoja na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la FEMA Sauda Simba Kilumanga akiangalia bidhaa za jarida la FEMA wakati wa hafla ya kutimiza miaka 20 ya Shirika la FEMA jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy pamoja na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la FEMA Sauda Simba Kilumanga wakiingia ukumbini tayari kuanza   ya kutimiza miaka 20 ya Shirika la FEMA jana jijini Dar es Salaam.   

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka walimu wa kuu wa Shule za Sekondari Nchini kushirikiana na Shirika la FEMA Hip kuanzisha club za vijana katika shule zao ili kutoa fursa za vijana mashuleni kupata elimu ya Afya ya uzazi na kujitambua.

Waziri Ummy amesema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo ambalo kwasasa lina uwezo wa kuwafikia vijana 15,000 kila mwezi na kuwalimisha masuala mbalimbali ya kiafya ikiwemo kujikinga na maabukizi ya ukimwi.

Aidha Waziri Ummy aliongeza kuwa yeye amekuwa mdau mkubwa katika kuhakikisha vijana Nchini wanapata elimu ya uzazi nchini ikiwezekana hata mtoto wa darasa la tano na kuwafanya kutambua angalau kulinda mwili wao kwani siku hizi watoto wanapevuka katika umri mdogo.

Aliongeza kuwa mwelekeo wa Serikali ni kuwa na uchumi wakati lakini hatuwezi kufikia hapo kama bado kati ya wasichana 100 wasichana 27 wanapata mimba katika umri mdogo hivyo kuwa na mzunguko wa umasikini usio kwisha.

Aliwapongeza FEMA kwa kuanza kupunguza masuala ya elimu ya Afya na uzazi nakuanza kujielekeza katika masuala ya uwezeshaji wa wa vijana kiuchumi kwani kama utampatia elimu bila kuwawezesha kiuchumi matatizo yao yanabaki palepale.

Amelitaka shirika hilo kuanzisha pia masuala ya elimu ya lishe kwa kuwa Tanzania kwasasa inakabiliwa na tatizo la udumavu ambapo kila watoto 100 watoto 34 wenye umri chini ya miaka 5 wamedumaa.

Shirika la FEMA limitimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na limekuwa likijihusisha na utoaji na uhamasishaji vijana kujikinga na ukimwi, kuwapa matumaini wa wathirika wa ugonjwa wa ukimwi, kutoa elimu ya Afya uzazi kwa vijana, kuwawezesha vijana kubuni namna bora za kujiwezesha kiuchumi kupitia club za FEMA Hip mashuleni lakini pia kwa kupitia vyombo vya habari.

No comments: