Advertisements

Saturday, June 22, 2019

KATIBU MKUU MASSAWE AHIMIZA USHIRIKIANO KWA WATUMISH

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akizungumza na Watumishi wa ofisi hiyo (hawapo pichani) alipokutana nao kujadili utendaji kazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Ofisi hiyo, Bw. Peter Kalonga akieleza jambo kwa watumishi wa Ofisi hiyo (hawapo pichani) ikiwa ni sehemu ya maaadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi hiyo wakifuatilia maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (hayupo pichani) walipokutana Jijini Dodoma.

Na; Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe amewaasa watumishi wa ofisi hiyo kufanyakazi kwa ushirikiano ili waweze kutumiza malengo waliyojiwekea.

Hayo ameyasema wakati alipokutana na watumishi wa ofisi yake Dodoma kwa lengo la kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika kila mwaka kuanzia Juni 16 hadi 23 kwa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kwa lengo la kuonesha mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya nchi zao na Bara la Afrika kwa ujumla ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni;

“Uhusiano kati ya uwekezaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji: Jenga utamaduni wa Utawala bora, matumizi ya TEHAMA na Ubunifu katika utoaji wa huduma jumuishi.”

Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo ipo kisheria Katibu Mkuu huyo alisema kuwa Ofisi hiyo ina majukumu makubwa ya kiutendaji hivyo watumishi wanawajibu wa kufanyakazi kwa kushirikiana na kujenga umoja.

“Ushirikiano katika kazi ni muhimu na husaidia kuboresha mifumo ya kiutendaji ikiwemo kuwa na mikakati endelevu ya ofisi, mawasiliano mazuri, kujenga mahusiano mazuri na wadau na kutoa huduma bora kwa wananchi,” alisema Massawe.

Sambamba na hilo aliwasihi watumishi wa ofisi hiyo kufanyakazi kwa bidii, weledi, uzalendo na kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao na utoaji wa huduma kwa wadau na wananchi.

Pia amewashauri watumishi hao kuepukana na vitendo vya rushwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na maadili ya Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia haki na usawa.

Aidha, Katibu Mkuu alikutana na kufanya kikao na wadau mbalimbali wa nje na alipokea maoni na mrejesho wa huduma zinazotolewa na Ofisi ya Waziri kuhusu sekta ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira, Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii na masuala ya Vyama vya Wafanyakazi.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Peter Kalonga aliafiki yaliyosemwa na kuahidi kuahidi kufanyia kazi maagizo hayo ikiwemo suala la ushirikiano na mawasiliano katika utendaji kazi baina ya watumishi ili kuimarisha mshikamano baina ya watumishi.

Kwa upande wake alisema kuwa kikao hiko kimewezesha watumishi wa ofisi hiyo kubadilishana taarifa zaidi za kiutendaji na kitasaidia kuimarisha ushirikiano baina yao
Mmoja wa Watumishi wa Ofisi hiyo Bi. Grace Kigula akielezea baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji walipokutana na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe alipokutana nao kusikiliza maoni na changamoto wazokabiliana nazo katika utendaji kazi wao.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (katikati) akifafanua jambo kwa wadau (hawapo pichani) alipokutana nao kwa lengo la kujadiliana pamoja na kusikiliza maoni, ushauri na changamoto wanazokutana nazo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2019. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Johanes Majura na kulia ni Mwanasheria kutoka Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Suzan Ndomba.
Naibu Katibu Mkuu, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Johanes Majura (kushoto) akifafanua jambo kuhusu masuala ya vyama vya wafanyakazi wakati wa mkutano huo uliofanyika ghorofa la PSSSF, Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe.
Mwanasheria kutoka Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Suzan Ndomba akielezea kuhusu baadhi ya Sheria zinazowaongoza Waajiri nchini wakati wa kikao na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (katikati) alipokutana na wadau mbalimbali wa ofisi hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Johanes Majura
Baadhi ya wadau wakifuatilia maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (haupo pichani) walipokutana kujadili masuala mbalimbali kuhusu sekta ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira, Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii na masuala ya Vyama vya Wafanyakazi
Mmoja wa wadau kutoka Kampuni ya RECO Engineering Ltd, Bw. Abubakar Mukadam akichangia mada kuhusu masuala ya vibali vya kazi walipokutana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (haupo pichani) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Sehemu ya ya wadau wakifuatilia maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (haupo pichani) walipokutana kujadili masuala mbalimbali kuhusu sekta ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira, Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii na masuala ya Vyama vya Wafanyakazi.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU

No comments: