
Mwanafunzi huyo aliyefahamika kwa jina la Almaz Derese, ambaye anatokea eneo la Metu Kaskazini mwa nchi ya Ethiopia alijifungua mtoto wa kiume katika hospitali ya Metu nchini Ethiopia.
Kwa mujibu wa msichana huyo, awali alifikiri ataweza kufanya mtihani huo kabla ya kujifungua lakini ilishindikana baada ya kuhairishwa kwa sababu ya mfungo wa Ramadhani.
“Nilienda kujifungua siku Jumatatu asubuhi muda mfupi kabla ya mtihani wa kwanza kuanza,” Almaz aliliambia Shirika la Habari la Uingereza (BBC).
“Kwa sababu nilikuwa nawaza kuhusu mtihani wangu, sikupata shida katika kujifungua,” alisisitiza Almaz.
Akiwa katika hospitali hiyo, Almaz alifanya mitihani ya masomo matatu ikiwamo ya Kiingereza, Amharic na Hisabati huku akiwa na matumaini kwama iliyobaki atafanya shuleni baada ya siku mbili. MWANANCHI
No comments:
Post a Comment