
GARI ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, jana lilipata ajali mbaya iliyosababishwa na mtoto wa dereva wake anayedaiwa ‘kuliiba’ na kutoka nalo. Imeelezwa kuwa deveva wa mkuu wa mkoa huyo na mkewe walizimia baada ya kusikia tukio hilo.
“Wakati akizungumza na mgeni huyo mtoto wake mwenye umri wa miaka 24 alilichukua gari hilo bila ruhusa ya baba yake na kuondoka nalo.
“Alipofika eneo la kanisani lilimshinda na kuingia mtaroni. Hii ajali ni ya kizembe huyu kijana alikuwa spidi kubwa,” alisema RPC Ndaki na kuongeza kwamba madhara ni makubwa katika ajali hiyo kwani utengenezaji wake sio chini ya Sh milioni 80.
Aidha, alisema kijana huyo aliumia na kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
“Baba yake alipofika katika tukio hilo alizimia na mkewe alipopata habari za ajali hiyo naye alipoteza fahamu. Wote wamepelekwa hospitali,” alisema GPL

No comments:
Post a Comment