ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 23, 2019

Rais Magufuli amesema kwamba Mradi wa Coco beach wa Bilioni 14 unazuiwa na SHERIA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA YA MWAKA 2004


SHERIA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA YA MWAKA 2004 (NA.20 YA 2004)
Ulinzi na usimamizi wa mito, miambao ya mito, maziwa au
miambao ya maziwa na fukwe.
55 (1) Bila kuathiri masharti yoyote ya sheria nyingine yoyote iliyotungwa na Bunge, Baraza na mamlaka za serikali za mitaa zinazohusika na masuala ya mazingira, zitatoa miongozo na kubainisha hatua za kilinda, kingo za mito, mito, maziwa au miambao ya maziwa na fukwe.
(2) Pale ambapo miongozo na hatua zitakapokuwa zimebainishwa kufuatia kifungu cha (1), litakuwa ni kosa kufanya shughuli yoyote kati ya hizi zifuatazo bila kwanza kupata ruhusa au kibali kilichotolewa na Waziri-
(a) Kutumia, kusimika, kujenga, kuweka, kubadili, kuongeza,
kuondoa, au kubomoa jengo au umbile kwenye au chini ya bahari au fukwe asili za ziwa, ukingo wa mto au bwawa;
(b) Kufukua, kuchoronga, kutoboa au kuharibu fukwe za bahari au 43 ziwa asili, kingo za mto au kisima cha maji au bwawa; ....

No comments: