Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Elias Kwandikwa akichomelea chuma kuashiria kuanza kwa ujenzi wa kivuko kipya cha Mafia Nyamisati. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 sawa na tani 100, kinajengwa kwa shilingi bilioni 5.3 za Kitanzania na kitakamilika ifikapo mwezi Februari mwakani.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Elias Kwandikwa katikati akipewa maelezo kuhusu namna kivuko cha Mafisa Nyamisati kitakavyojengwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Songoro Salehe Songoro wakati alipokua akizindua ujenzi wa kivuko hicho Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle kushoto akisoma taarifa fupi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Mhandisi Elias Kwandikwa wa (pili kushoto)wakati alipokua akizindua ujenzi wa kivuko kipya cha Mafia Nyamisati, tukio lililofanyika katika yadi ya Songoro Kigamboni. Kutoka kulia ni Lazaro Vazuri na mbunge wa Mafia Mbaraka Dau

No comments:
Post a Comment