Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango umefunguliwa leo kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Jengo la Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Arusha na utafanyika kuanzia tarehe 7 hadi 12 Oktoba 2019. Mkutano huo unaanza na vikao vya awali ambavyo ni kikao cha Maafisa Waandamizi kinachofanyika tarehe 7 na 8 Oktoba 2019 na utafuatiwa na kikao ngazi ya Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 9 na 10, na kumalizia na ngazi ya Mawaziri tarehe 11 na 12 Oktoba 2019. Pichani; Wapili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kikao cha ngazi ya Wataalamu na Afisa Mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Jamhuri ya Rwanda, Bw. Emmanuel Kamugisha akiongoza kikao hicho. Pembeni ya Mwenyekiti wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Christophe Bazivamo, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Forodha na Biashara, Bw. Keneth Bagamuhunda, na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Raphael Kanoth. Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia majadiliano katika kikao cha ngazi ya wataalamu. Wapili kushoto ni Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Balozi Stephen Mbundi, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, Bw. Benard Haule, wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Bi. Caroline Chipeta na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. Gerald Mweli. Ujumbe wa Tanzania ukifatilia majadiliano katika kikao cha ngazi ya wataalamu. Mkutano ukiendelea. |
No comments:
Post a Comment