Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa miaka miwili na CABBIES DO KILIMANJARO 2019 ya jijini London wa kuwa mabalozi wa utalii wa hiari ukuwa ni mkakati wa kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Uingereza.
Mkurugenzi wa TTB Devota Mdachi na John Dillane wa CABBIES Do KILIMANJAEO wakitiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ambao una sharia na taratibu ambazo zinatakiwa kufuatwa wakati wa wakutekeleza jukumu yao ya kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia matukio mbalimbali atakayokuwa yanafanywa na mabalozi hao nchini Uingereza.
Mkurugenzi wa TTB Devota Mdachi na John Dillane wa CABBIES Do KILIMANJAEO wakipongezana mara baada ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa miaka miwili na CABBIES DO KILIMANJARO 2019 ya jijini London wa kuwa mabalozi wa utalii wa hiari ukuwa ni mkakati wa kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Uingereza.
Cabbies Do Kilimanjaro ni kampeni iliyofanywa na Timu ya Madereva Tax wanne wanaojulikana kama London Black Taxi Drivers kwa lengo la kuutangaza na kuwahamasisha wananchi wa London kuja Tanzania kupanda Mlima Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment