ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 5, 2019

SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUTAFUTA SULUHU YA SUMUKUVU

Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akizunumza na wadau wa mkutano unaojadili namna ya kudhibiti Sumukuvu, wanaotoka katika nchi 15 za Afrika katika mkutano unaofanyika katika Hotel ya Mount Meru Jijini Arusha leo Novemba 4, 2019.
Washiriki wa Mkutano unaojadili namna ya kudhibiti Sumukuvu wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa Kilimo Mhe.Josephat Hasunga.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Afrika wa kudhibiti Sumukuvu (Alfasafe) kwenye vyakula wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akisisitiza mkakati wa serikali katika kukabiliana na Sumukuvu nchini, uliofanyika katika Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha tarehe 4 Novemba 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akifuatilia mawasilisho mbalimbali ya washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Afrika wa kudhibiti Sumukuvu (Alfasafe) kwenye vyakula uliofanyika katika Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha tarehe 4 Novemba 2019. 
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Afrika wa kudhibiti Sumukuvu (Alfasafe) kwenye vyakula wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akisisitiza mkakati wa serikali katika kukabiliana na Sumukuvu nchini, uliofanyika katika Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha tarehe 4 Novemba 2019

NA VERO IGNATUS, ARUSHA.

WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga amewataka wakulima kuchukua hatua kudhibiti Sumukuvu ambayo imekua ikiathiri mazao tangu yanapokua shambani na baada ya kuvunwa.

Udhibiti w aSumukuvu utasaidia kuondokana na sumu hiyo yenye madhara yasababishayo saratani na hatimaye kifo.

Akizungumza katika mkutano wa wadau hao leo Novemba 4, 2019 katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha, Mhe.Hasunga amesema kuwa serikali imeanza kushirikiana na wadau wakiwemo wakulima ili kutafuta namna na kuyakinga mazao yao dhidi ya sumukuvu na tayari wamekuja na dawa itakayowasaidia kudhibiti sumu hiyo kabla na baada ya mazao kuvunwa.

Amesema mkutano huo unaojadili namna ya kudhibiti Sumukuvu ili kuona ni hatua gani zichukuliwe, kuhakikisha kwamba wanapambana na ugonjwa huo sambamba na kutoa hamasa na elimu kwa wakulima kuhusu madhara ya ugonjwa huo huo na namna ya kuutokomeza.

Mhe. Hasunga amesema tayari Serikali imekuja na mkakati uliozinduliwa wakati wa maonesho ya nanenane mkoani Simiyu na umeshaanza kutekelezwa katika programu inayotambulika kama TANIPAC ambapo moja ya mambo yanayotekelezwa katika mradi huo ni kuhakikisha kuwa wanajenga maghala, kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuepukana na sumukuvu.

Aidha amesema Utafiti uliofanywa na wataalamu wa nchi mbalimbali unaonyesha kwamba takribani asilimia 20 hadi 40 ya mazao mbalimbali ya nafaka yanaathiriwa na ugonjwa wa sumukuvu.

Waziri amewataka Watafiti kufanya utafiti juu ya sumukuvu na kuangalia hali halisi ya tatizo hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa watafiti itakayosaidia kuchukua hatua zaidi.

Mratibu wa Utekelezaji Mradi wa Kudhibiti Sumu kuvu nchini,Clepin Josephat ,Mtaalamu amesema kuwa mwaka 2016 baadhi ya watu walifariki kutokana na sumu kuvu ,ambayo haionekani na haishikiki hivyo serikali ipo kwenye mpango wa kujenga maabara kubwa ya kilimo itakayosaidia kukabiliana na tatizo hilo.

Mtafiti Mwandamizi wa Teknolojia ya kudhibiti sumu kuvu ya Aflasafe kutoka shirika la IITA Ranajit Bandyopadhyay ,amesema kuwa baada ya utafiti wao na kupata dawa ya kudhibiti sumu kuvu wamekuja na mikakati ya kusambaza taifiti hiyo na dawa ili iweze kusaidia wakulima baada ya kukaa katika maktaba .

Kwa mujihu wa takwimu za mwaka 2017 za Shirika la chakula na Kilimo Duniani,(FAO)Tanzania ininazalisha tani milioni 6 za mahindi,ipia inazalisha zaidi ya tani milioni 1 za karanga .

No comments: