Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede akipokea tuzo ya ushindi wa jumla ya uandaaji bora wa taarifa za hesabu kati ya taasisi, wakala, kampuni na mashirika mbalimbali kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaabani wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede akionyesha tuzo ya mshindi wa kwanza ya uandaaji bora wa taarifa za hesabu katika kipengele cha Wakala wa Serikali aliyopokea kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaabani wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede (katikati aliyeshika tuzo) akiwa na Naibu Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo (wa pili kushoto kwake) pamoja na watumishi wa Idara ya Fedha mara baada ya kupokea tuzo mbili za uandaaji bora wa taarifa za hesabu wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju jijini Dar es Salaam


No comments:
Post a Comment