Advertisements

Thursday, February 20, 2020

Dawa ya Chloroquine kutibu corona

Beijing, China. Dawa ya malaria aina ya chloroquine imedhibitisha kutibu virusi vya corona (covid-19)

Dawa hiyo iliyokuwa ikitumika zaidi kutibu ugonjwa wa malaria katika miaka ya 1980 na 1980 imeonyesha kutibu virusi hivyo baada ya kufanyiwa utafiti na wataalam wa afya wa nchi hiyo.

Wizara ya Afya sayansi na teknolojia ya China, ilisema “chloroquine imethibitisha inaweza kutibu corona lakini pia ikakinga ugonjwa wa maralia kwa miongo kadhaa sasa.”

Shirika la habari la Xinhua limeripoti kuwa chloroquine imekuwa ikitumika kwa zaidi ya hospitali 10 ikiwamo moja iliyopo katika mji mkuu wa Beijing na mbili katika majimbo mengine.

Kwa mujibu wa Xinhua dawa hizo zimeonyesha ufanisi mzuri.

No comments: