Advertisements

Thursday, February 20, 2020

WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA MAREKANI, UMOJA WA ULAYA, ASEMA NCHI IPO SALAMA, UCHAGUZI UTAKUWA HURU NA HAKI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani, Umoja wa Ulaya (EU), Angola na Kuwait nchini, na kuwahakikishia kuwa Tanzania ipo salama, na pia katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu utakuwa wa huru na haki.
Akizungumza na mabalozi hao waliofika kwa wakati tofauti ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo, Simbachawene amesema vyombo vyake vinaendelea kufanya kazi kwa weledi katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao nchini.
“Tunatarajia kufanya uchaguzi mwaka huu, na swali lako hali ya usalama nchini, tunawahakikishia nchi ipo salama, ulinzi utaimarishwa na uchaguzi utakua wa huru na haki,” alisema Simbachawene.
Pia Waziri Simbachawene aliwahakikishia shirikiano zaidi kati ya Wizara yake na mabalozi hao katika masuala mbalimbali ya utendaji kazi.
“Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yangu imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio hapa nchini,” alisema Simbachawene
Simbachawene aliwashuru mabalozi hao kwa kumtembelea, na aliwataka wawe huru muda wowote wanapohitaji kumuona wanakaribishwa ofisini kwake.
“Najisikia furaha kwa ujio wenu na karibuni sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Simbachawene.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto) akimkaribisha Kaimu Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Imni Patterson, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, leo. Simbachawene alimwakikishia Balozi huyo Tanzania ipo salama na kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, utakuwa wa huru na haki.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akizungumza na Balozi wa Umoja wa Ulaya, Manfredo Fanti, masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Umoja huo na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ndogo ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Alsehaijan, baada ya kumaliza kikao chao kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akizungumza na Balozi wa Angola, Sandro De-Oliveira, masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ndogo ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akizungumza na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Imni Patterson, masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ndogo ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akimsindikiza Balozi wa Umoja wa Ulaya, Manfredo Fanti, baada ya mzungumzo yao ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ndogo ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akizungumza na Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Alsehaijan, masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ndogo ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments: