ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 19, 2020

Makamu wa Rais Akutwa na Corona

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, Riek Machar na mkewe, Angelina Teny, ambaye ni Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo wamekutwa na maambukizi ya Covid-19 jana (Jumatatu).

Taarifa zilizopo zinasema watu hao walipata maambukizi hayo baada ya kukutana na watu walio katika tume maalum ya kupambana na ugonjwa huo.

Pia wafanyakazi kadhaa wa ofisi za viongozi hao, wakiwemo walinzi, pia wamepata maambukizi hayo japokuwa majina yao hayakuchapishwa.

No comments: