Katika kuhakikisha mapambano dhidi ya KifuaKikuu TB yanaendelea leo Mei 20, 2020, Zahanati ya Buigiri - Chamwino jijini Dodoma imemkabidhiwa Hadubini za Kisasa (LED Microscope) 57 kwa ajili ya vituo vya huduma za Afya mkoa wa jiji la Dodoma. Lengo ni kuimarisha huduma za upimaji na ugunduzi wa TB, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu amesema wakati akimkabidhi RC Dodoma Dkt. Mahenge
Hadubini hizi ni sehemu ya Hadubini (Microscope) 941 zilizonunuliwa na Wizara ya Afya kwa thamani ya Tsh.bilioni 3.3 ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya 5 chini ya Rais Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ili kuboresha huduma za Afya nchini. "Ni faraja kuona kuwa Jitihada zetu zinazaa matunda ikiwemo
kupungua kwa maambukizi mapya ya wagonjwa wa TB kwa mwaka kutoka wagonjwa 160,000 (2015) hadi 142,000. Kupungua kwa vifo vitokanavyo na TB kwa mwaka kutoka vifo 30,000 (2015) hadi vifo 22,000". Amesema Waziri Ummy. Pia Waziri huyo ameishukuru GlobalFund kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kutokomeza maradhi hayo.
Pamoja na kuendelea na mapambano dhidi ya COVID19, Kipaumbele cha Wizara sasa ni kuhakikisha Mwendelezo wa huduma muhimu za Afya (Continuity of Essential Health Services) ikiwemo Huduma za Mama na Mtoto (RCH), Chanjo, Udhibiti wa magonjwa mengine kama TB, Malaria, HIV


No comments:
Post a Comment