
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Kenan Laban Kihongesi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha akitoa hotuba ya kufungua mafunzo hayo.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba yake.

Mhe. Kihongozi akiagana na Bw. Mshomba (wakwanza kushoto), Dkt. Omary (wapili kulia) na Mkuu wa jopo la wawezeshaji wa Mafunzo hayo Dkt. Robert Mhina.
MKUU wa Wilaya ya Arusha Mhe. Kenan Laban Kihongosi, leo Juni 24, 2020 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha amefungua mafunzo ya uelimishaji wa tathmini za ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na watoa huduma ya afya wa kanda ya kaskazini, yanayofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC jijini Arusha.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na haya ndiyo aliyoyasema wakati akifungua mafunzo hayo ya siku tano.
No comments:
Post a Comment