ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 12, 2020

Nimerudi Yanga na nguvu mpya



Mwamvita Mtanda ,Dar es Salaam, MTANZANIA

BAADA ya Sintofahamu ya takaribani wiki tatu kuhusu kurejea kwa kocha Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael, hatimaye amewasili jana na atajiunga na kikosi chake leo.

Eymael hataki kupoteza muda , leo hii ataondoka na ndeki ya Shirika la Precision, kulekea Sinyanga kukutana wachezaji wake, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, dhidi ya Mwadu.

Licha ya kuwa Mbelgiji huyo alitua saa 1:30 na Ndege ya Shirika la Ethiopia, lakini uongozi wa Yanga amempotezea na hakuna hata mmoja aliyefika kumpokea.

Akizungumza na MTANZANIA jana, baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Eymael alisema, jambo la kushukuru kwake ni kuwa amerudi salama na kuwahi mechi yao na Mwadui.

Alipoulizwa kuusu kutopokelea na uongozi wa Yanga, Mbelgiji huyo alisema, hakutarajia kama wasingekuja kumpokea lakini inawezekana wamebanwa na majukumu mengine, lakini ataweza kufika nyumbani kwake.

“Siwezi kufahamu kwanini hawakuja, lakini kila jambo linakwenda kwa ratiba, yawezekana wamebanwa lakini haiweze kufanya nisifike nyumbani.

“Nimepambana sana kurudi niwahi kazi yangu, pia kuona wachezaji wangu wakiwa uwanjani Jumamosi, siwazi mengine, nawaza kufanya kazi yangu iwe nzuri hasa majukumu tuliyonayo,”alisema Eymael.

Eymael alisema amerudi na nguvu mpya kuhakikisha kuwa timu yake inafanikiwa kufanya vyema, hasa katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam, pia kumaliza Ligi katika nafasi ya pili ambayo itawawezesha kushiriki michuano ya shirikisho ya kimataifa.

Mbelgiji huyo aliongeza kuwa, ataanza kazi rasmi ya kukinoa kikosi chake akifika Shinyanga, ambapo ataongoza mazoezi ya asubuhi Ijumaa asubuhi.

MTANZANIA lilimsaka, Ofisa Habari wa timu hiyo, Hassan Bumbuli, ili kufahamu sababu iliyowakwamisha kuja kumpokea Kocha wao.

Bumbuli alisema, hakukuwa na ulazima wa wao kwenda kumpokelea, kwa kuwa kocha huyo tayari anayafahamu mazingira ya Tanzania, hasa kutoka uwanjani wa ndege hadi nyumbani kwake Mikocheni.

“ Sioni kama kuna tatizo eti hakuja kupokelewa, sio mgeni anapafahamu kwake, hivyo tulikuwa tunaamini angeweza kufika,”alisema Bumbuli.

Kocha huyo alitua na mabagi matano ya vifaa mbali mbali vya michezo, baada ya kuona mapunguvu katika vifaa wanavyotumia sasa.

Pia Mbelgiji huyo aliambatana na mke wake, Patricia Abbruzzesse Eymael, ambaye alifunga naye ndoa hivi karibuni.

“Nafurahi sana kuja Tanzania nikiwa nimeambatana na mume wangu, mimi nishabiki wa Yanga, naisapoti pia namsapoti Eymael afanye kazi nzuri.

Natamanini tuishi sana Tanzania, lakini inategemea na mkataba wake na Yanga kama utaendelea itakuwa furaha zaidi kwetu,”alisema Patricia.

No comments: