Advertisements

Saturday, August 15, 2020

HAKUNA SABABU YA KUAGIZA MAZIWA KUTOKA NJE YA NCHI-WAZIRI MPINA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina akizungumza wakati wa ziara yake katika kiwanda cha Maziwa cha
Tanga Freshi Jijini Tanga kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Tanga Fresh
Inocent Mushi kulia ni Mwenyekiti wa cha ushirika wa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoa wa
Tanga (TDCU) Hamid Mzee
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina akizungumza wakati wa ziara yake kwenye kiwanda cha Maziwa cha Tanga fresh Jijini Tanga
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (TADB) Japhet Justine akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mtendaji Mkuu wa Tanga Fresh Inocent Mushi akitoa taarifa ya kiwanda hicho kwa Waziri Mpina ambaye amekaa kulia
Mwenyekiti wa chama cha ushirika wa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoa wa
Tanga (TDCU) Hamid Mzee akieleza jambo wakati wa ziara hiyo
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina amesema hakuna sababu ya kuagizwa maziwa kutoka nje ya nchi kutokana na
uwepo wa mifugo ya kutosha ambayo ikiwekewa utaratibu mzuri itajitosheleza
kuzalisha bidhaa hiyo kwa kiasi cha kutosha.

Mpina aliyasema hayo wakati wa ziara
yake kwenye kiwanda cha kuzalisha Maziwa cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga
aliyoambatana na watendaji mbalimbali.

Alisema kwani hivi sasa maziwa hapa
nchini ni mengi kutokana na uwepo wa viwanda vya kuzalisha maziwa kwa njia ya
mchakato ambavyo vimetakiwa kuzalisha kwa wingi na kukuza soko ili kukwepa
uingizwaji wa maziwa kutoka nje ya nchi.

“Tumeweza kuona changamoto na
fursa mlizonazo kuanzia kwenye mifugo mpaka uzalishaji na masoko, nawapongeza
sana Tanga fresh kwasasa kwa kazi nzuri mnayofanya, hakuna sababu ya watu
kuingiza maziwa kutoka nje ya nchi wakati tuna mifugo ya kutosha kutupatia
maziwa” alisema Mpina.

Waziri Mpina aliutaka uongozi wa
kiwanda hicho kununua maziwa kwa wafugaji kwa bei itakayomfanya mfugaji
kunufaika na uzalishaji wa mifugo yake hatua inayotokana na kutokuwepo kwa bei
elekezi ya kununulia maziwa kwa mfugaji.

“Changamoto nyingine ni hii ya
bei, tulipotangaza ununuzi wa maziwa hatukuweka bei elekezi lakini ningependa
bei ya maziwa kwa mfugaji iwe ni shilingi mia nane kwa lita, nitafurahi na
nitapenda kwa kila kiwanda kinunue maziwa kwa mfugaji kwa bei hiyo”
alibainisha.

Akifafanua kuhusu changamoto ya
magonjwa kwa mifugo, Waziri Mpina alisema ili kupata maziwa kwa wingi na yenye
ubora ipo haja ya kuangalia ukuaji wa mifugo hususani katika magonjwa, lishe na
chanjo pamoja na mazingira wanayoishi.

“Mkurugenzi wa nyanja za
malisho muende muwatembelee wafugaji kule kwenye maeneo yao muone maeneo
wanayofugia, vyakula wanavyoipatia mifugo na hata chanjo ili kuwakinga na
magonjwa” alisema Mpina.


Awali akizungumza wakati wa ziara
hiyo Mwenyekiti wa chama cha ushirika wa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoa wa
Tanga (TDCU) Hamid Mzee alisema changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakumba wafugaji
ni migogoro ya ardhi na kueleza kwamba wanatakiwa kuweka mpango mkakati ili
kutengeneza maligafi kwa wingi na kukwepa ukosefu wa bidhaa hiyo.

Mwenyekiti huyo pia aliiomba
serikali kuangalia kwa ukaribu wafugaji na kuwawezesha kuzalisha kwa tija huku
wakinufaika na mifugo yao kwani tatizo la uzalishaji lililokuwepo awali kwa
sasa limepungua na kufanya soko kuongezeka.

“Migogoro ya kunyang’ anyana
ardhi ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita hatukuweza kuzalisha mitamba ya
kutosha na kusababisha tatizo la kuoungua kwa uzalishaji lakini sasa soko
limerudi tena, niiombe serikali ijitahidi kuliangalia hili suala ili wafugaji
wetu wanufaike na mazao yao ya mifugo” Alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha alisema pia changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakumba wafugaji
ni migogoro ya ardhi na kueleza kwamba wanatakiwa kuweka mpango mkakati ili
kutengeneza maligafi kwa wingi na kukwepa ukosefu wa bidhaa hiyo.

Mwenyekiti huyo pia aliiomba
serikali kuangalia kwa ukaribu wafugaji na kuwawezesha kuzalisha kwa tija huku
wakinufaika na mifugo yao kwani tatizo la uzalishaji lililokuwepo awali kwa
sasa limepungua na kufanya soko kuongezeka.



“Migogoro ya kunyang’ anyana
ardhi ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita hatukuweza kuzalisha mitamba ya
kutosha na kusababisha tatizo la kuoungua kwa uzalishaji lakini sasa soko
limerudi tena, niiombe serikali ijitahidi kuliangalia hili suala ili wafugaji
wetu wanufaike na mazao yao ya mifugo” Alisema Mwenyekiti huyo.

No comments: