Advertisements

Wednesday, December 2, 2020

AFISA TAKUKURU IRINGA AMPIGA KOFI MWALIMU MJAUZITO KISA DAFTARI LA MAHUDHURIO

katibu wa chama cha walimu wilaya ya kilolo (CWT) wilaya ya Kilolo Anthony Mang’waru akiongea na waandishi wa habari juu ya sakata la kupigwa kwa mwalimu.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

CHAMA cha walimu wilaya ya
kilolo kimeanzima kutoshikiana na taasisi ya kuzia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)
mkoa wa Iringa kutokana na madai kuwa mmoja ya maafisa wake kupiga mwalimu wa
shule ya msingi Kitelewasi akiwa kwenye majukumu yake.

Akizungumza na waandishi wa
habari mwenyekiti wa chama cha walimu wilaya ya Kilolo Mtemi Mgalula alisema kuwa wamefedheheshwa na kitendo cha
afisa TAKUKURU kumpiga mwalimu kibao
akiwa anatekeleza majukumu yake akiwa kazini.

Alisema kuwa wameanzimia
kumpeleka mahakamani afisa huyo wa TAKUKURU mkoa wa Iringa kutokana na
kuchukizwa na kitendo hicho alicho kifanya kisichokuwa cha uungwana kwa mwalimu
huyo wa shule ya msingi Kitelewasi.

Mgalula aliongeza kuwa
wameanzimia kutoshirikiana kwa jambo lolote lile na taasisi ya kuzia na
kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa ili kukomesha vitendo hivyo
ambavyo vimekuwa vikiwazalilisha walimu wawapo kazini.

“Hakuna jambo au tukio lolote
ambao walimu wa wilaya ya Kilolo watashirikiana na taasisi ya kuzia na
kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa hadi pale watakapojirekebisha na
kuacha kuwanyanyasa walimu wawapo kazini” alisema

Mgalula alisema kuwa wataanza
kutoa elimu ya walimu kujilinda kwa kuwa sheria za nchi zinarusu kujilinda ili
waache kunyanyashwa na kufanya kazi yao kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao na
kuhakikisha wanatoa elimu bora kwa wanafunzi wanaowafundisha.

Hakuna haki ya mwalimu huyu
itakayopotea kwa kuwa tunajilinda na tunaviongozi wa mkoa ambao wanathamini
kazi za walimu hivyo tunauhakika kuwa mwalimu huyu atapata haki yake na huyo
afisa tunamkaribisha aje tuongee lakini lazima haki ya mwalimu ipatikane.

Akieleza tukio hilo mwalimu
Latifa Kitosi ndiye anayetajwa kupigwa na afisa TAKUKURU alisema kuwa maafisa
hao walifika ofisi na kuomba daftari la mahudhurio ya darasa la sita la mikondo
yote miwili lakini kwa halaka daftari la mahudhurio lililokuwepo jirani ni
daftari la mkondo B wakati mahitaji ya maafisa hao wa TAKUKURU walikuwa
wanahitaji daftari la mkondo A

Alisema kutokana na daftari la
mkondo A yaliibuka majibizano baina ya maafisa hao wa TAKUKURU na walimu
waliokuwepo katika ofisi hiyo na mmoja ya maafisa hao kupiga kibao mwalimu
ambaye ni mjamzito na kisha kulichukua daftari hilo la mahudhurio na kumtaka
mwalimu huyo kufika katika ofisi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo kwa mahojiano
zaidi.

Kitosi alisema kuwa maafisa hao
walimtuhumu yeye na mwalimu mkuu msaidizi kuwa kuharibu ushahidi wa mahudhurio
ya mwanafunzi kutokana na kuchelewesha
daftari la mahudhurio la mkondo A ambalo hasa maafisa hao walikuwa wanalihitaji
kwa ajili ya kuangalia mahudhurio ya mmoja ya wanafunzi wa darasa hilo.

Aliongeza kuwa chanzo cha hayo
yote yanatokana na mwanafunzi kutohudhuria masomo kwa kipindi cha siku kumi na
nne bila taarifa yoyote ile kwa uongozi wa shule hiyo ya kitelewasi.

Kwa upande wake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo Chako
Mdemu alisema kuwa mnamo tarehe 12
alipata ujumbe mfupi ukieleza kuwa kuna kila dalili za kutoroshwa kwa
mwanafunzi huyo kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufanya kazi za
ndani kama ambavyo imekuwa ikifanyike kwa wanafunzi wengine walivyokuwa
wanafanya miaka ya zamani.

Mdemu alisema kuwa baada ya
kugundua tatizo hilo ndipo walipotoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ili kuweza
kuzuia kutoroshwa kwa mwanafunzi huyo wa darasa la sita katika shule ya
sekondari ya Kitelewasi wilayani kilolo mkoani Iringa.

Mwalimu mdemu alisema kuwa
kuanzia mzazi wake,dada yake na mwanafunzi mwenyewe walikiri kuandaa mikakati
ya kumtorosha mwanafunzi huyo kinyume na sheria za nchi na ndio kilikuwa chanzo
cha dada wa mwanafunzi huyo kupeleka keshi hiyo TAKUKURU.

Alisema kuwa maafisa hao wa
TAKUKURU hawakuwa wamejitambulisha wala kuandikisha kuwa wao ni maafisa TAKUKURU
hivyo ili kuwa ngumu kwa viongozi wa serikali ya kijiji na walimu kuwatambua
kuwa wao maafisa wa serikali na wameenda kwa kazi maalum.

Naye kamanda wa taasisi ya
kuzia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa,Domina Mkama akiri
kupigwa kofi kwa mwalimu huyo wa kike ambaye ni mjamzito kutokana na mazingira
ambayo walimu hao walikuwa wamemtengenezea afisa huyo hadi kutokea tukio hilo.

Mkama alisema baada ya kupigwa
kofi mwalimu huyo ndio daftari la mahudhurio lilitolewa na huyo mwalimu na
kuendelea na upelezi ambao maafisa hao walikuwa wanauhitaji kwa ajili ya
kuifanyia kazi ambayo walikuwa wanataka kuifanya.

Alisema kuwa serikali kwa
serikali hawawezi kugomba hivyo ameumba uongozi wa chama cha walimu wilaya ya
Kilolo kukaa meza moja kuhakikisha wanalimaliza tatizo hilo mara moja ili
kuendelea kushirikiana kama ilivyokuwa hapo awali.

Lakini pia katibu wa CWT wilaya
ya Kilolo Anthony Mang’waru alisisitiza kuwa hawataendelea kutoa ushirikiano na
taasisi ya kuzia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa hadi pale
watakapo kaa meza moja na kufikia muafaka na kusitisha vitendo hivyo vya
kuwanyanyasa walimu.

Tumesikitishwa sana na
tunalaani kitendo hicho cha kupigwa kwa mwalimu na kitendo ambacho sio cha
kiungwana kufanya tukio hilo na ambacho hakikubariki kabisa kwenye jamii yeyote
ile hapa nchini.

No comments: