ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 5, 2020

Magufuli Ateua Baraza la Mawaziri

RAIS John Magufuli, leo Desemba 5, 2020, ameteua baraza la mawaziri ambapo orodha hiyo imesomwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ni Elias Kwandikwa, Wizara Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ni Capt. Mst. George Mkuchika.

Wizara ya Ardhi ni William Lukuvi, Wizara ya Maji ni Juma Aweso, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ni Innocent Bashungwa, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ni Jenista Mhagama

Wizara ya Afya ni Dkt. Dorothy Gwajima, ambaye pia rais amemtea kuwa Mbunge, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji ni Prof. Kitila Mkumbo, Wizara ya Katiba na Sheria -ni. Dkt. Mwigulu Nchemba naWizara ya Elimu -niProf. Joyce Ndalichako.

Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni Mashimba Mashauri Ndaki, Wizara ya Maliasili na Utalii ni Dkt. Ndumbaro Damas Daniel, Ofisi ya Rais TAMISEMI ni. Selemani Jafo, Wizara ya Nishati ni Dkt. Medard Kalemani, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ni Leonard Chamuriho na Wizara ya Kilimo ni Prof. Adolf Mkenda.

Wizara ya Madini ni Dkt. Doto Biteko, Wizara ya Viwanda na Biashara ni Geoffrey Mwambe, na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni George Simbachawene

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ni Ummy Mwalimu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (wizara mpya) ni Dkt. Faustine Ndugulile

No comments: