Mwanamke huyo, kabla ya kifo chake anadaiwa pia alimnywesha sumu hiyo mtoto wake, Jordan Samson (3), ambaye hata hivyo alinusurika kifo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, alisema tukio hilo lilitokea Januari Mosi saa 8:00 usiku baada ya mama huyo kutoka katika mkesha wa Mwaka Mpya.
Jesca, akiwa na ndugu zake, wakitoka kwenye mkesha, alipata taarifa kuwa mume wake ameachiwa huru na baada ya kusikia hivyo, aliwaacha njiani aliokuwa nao na kuwahi nyumbani kisha akanywa sumu hiyo.
Malimi alisema baada ya ndugu zake kufika nyumbani, Jesca aliwaambia kuwa amekunywa sumu ya panya, ndipo walimpeleka hospitali ya Wilaya Nyakahanga na mtoto wake, ambapo mwanamke huyo alifariki dunia Januari 2, huku mtoto wake akipona.
Mumewe ambaye hakutajwa jina, alikuwa amefungwa kifungo cha miezi mitatu jela kutokana na mgogoro wa kifamilia.
GPL
No comments:
Post a Comment