Afisa wa juu jimbo la Georgia, Brad Raffensperger ametaja madai ya uongo ya Rais Donald Trump kuwa alipata ushindi wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana na kuita madai hayo “makosa yalio wazi”.
Kauli ya Raffensperger imekuja ikiwa ni siku moja tu tangu Trump alipomshinikiza katika mazungumzo ya simu yaliovuja kwamba “atafute” kura za kumuwezesha kupata ushindi kwenye jumbo hilo.
“Alizungumza sana. Na muda mwingi na sisi tukawa tunamsikiliza. Lakini nilichotaka kieleweke ni kuwa takwimu alizonazo ni za uwongo,” amesema Raffensperger.
Aidha, Raffensperger ameongeza kuwa wengi wa waliompigia kura Trump wamefariki dunia, hivyo alikuwa na kura hewa.
“Bwana Trump alikuwa na mamia na mamia ya watu waliompigia kura ambao walishafariki dunia. Tulipata majina ya watu wawili, huo ni mfano tu kwamba takwimu alizonazo sio sahihi,” aliongeza.
Gabriel Sterling, mkuu anayesimamia mfumo wa upigaji kura jimboni humo, amesema Jumatatu katika mkutano wa wanahabari kuwa madai ya Trump ni ya “uwongo mtupu”.
Trump amekosolewa vikali huku baadhi wakidai alichofanya ni sawa na kuingilia mchakato wa upigaji kura kinyume na sheria.
Wabunge wa Republican wanahofia kuwa hatua hiyo huenda ikadidimiza juhudi zao za kupata ushindi katika uchaguzi wa Maseneta wa jimbo la Georgia Jumanne.
Chanzo: Mtanzania
No comments:
Post a Comment