Wednesday, January 13, 2021

KILELE CHA SHEREHE ZA 57 MAPINDUZI ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa mara alipowasili viwanja vya Mnazi Mmoja katika kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,sherehe zilizofanyika leo
Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) katika kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,sherehe zilizofanyika leo viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwapungia mkono Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliopita katika viwavja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar leo katika Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwapungia mkono Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliopita katika viwavja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar leo katika Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Wananchi wafanyabishara wadogo wadogo wakiwa na bango lao kwa kumpomngeza Rais,Dk.Hussein Ali Mwinyi wakati walipopita katika maandamano ya kusherehekea kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar sherehe zilizofanyika leo viwanja vya Mnzi Mmoja Jijini Zanzibar.
Askari wa kikosi cha Polisi wakipita kwa mwendo wa Route March wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) katika kusherehekea kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar sherehe zilizofanyika leo viwanja vya Mnzi Mmoja Jijini Zanzibar.
Askari wa kikosi cha Polisi wa usalama barabarani wakipita kwa maonesho ya Amsha Amsha ya Mapinduzi mwendo wa Route March wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) katika kusherehekea kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar sherehe zilizofanyika leo viwanja vya Mnzi Mmoja Jijini Zanzibar.
Maonesho ya Amsha Amsha ya Mapinduzi mwendo wa Route March Gari za Vikosi vya Uluinzi wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) katika kusherehekea kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar sherehe zilizofanyika leo viwanja vya Mnzi Mmoja Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdalla mara alipowasili viwanja vya Mnazi Mmoja katika kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,sherehe zilizofanyika leo (wengine kutoka kulia) Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Amani Abeid Karume na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi (katikati) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdalla (wa pili kushoto) na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Amani Abeid Karume (kulia) mara alipowasili viwanja vya Mnazi Mmoja leo katika kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Amani Abeid Karume na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi (katikati) mara alipowasili viwanja vya Mnazi Mmoja leo katika kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) pamoja na Viongozi wa Kitaifa wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa wa Taifa wa Zanzibar,Afrika Mashariki na Wimbo wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wimbo Maalum wa “Sisi Sote Tumegomboka” katika katika kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar sherehe zilizofanyika leo viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar .
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa wa Taifa wa Zanzibar,Afrika Mashariki na Wimbo wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wimbo Maalum wa “Sisi Sote Tumegomboka” katika katika kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar sherehe zilizofanyika leo viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar .
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake fupi katika kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar sherehe zilizofanyika leo viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akitoa hutuba yake fupi kwa Wananchi wa Zanzibar katika Sherehe za kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar .
Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akitoa hutuba yake fupi katika Sherehe za kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.[Picha na Ikulu] 12/01/2021.

No comments: