Advertisements

Thursday, January 28, 2021

RAIS DKT. MWINYI ASHUHUDIA UTIAJI WA SAINI YA MAELEWANO (MoU) YA UJENZI WA BANDARI MANGAPWANI NA MJI WA KISASA BUMBWINI ZANZIBAR

BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa utiaji wa Saini ya Hati ya Maelewano (MoU) kuhusu Mpango Mkuu”Master Plan “ ya Ujenzi wa Bandari na Mji wa Kisasa Mangapwani na Bumbwini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbin wa Ikulu Jijini Zanzibar..
WAZIRI wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Rahma Kassim Ali, akizungumza wakati wa Utiaji Saini ya Maelewano (MoU) kuhusu Mpango Mkuu wa Ujenzi wa Bandari na Mji wa Kisasa Mangapwani na Bumbwini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 28-1-2021.
MKURUGENZI Mkuu wa Oman Investment Authority (OIA) Bw. Sheikh.Mohammed Al Taooqi, akizungunza kabla ya kutowa maelezo mafupi ya Ujenzi wa Bandari na Mji wa Kisasa Mangapwani na Bumbwini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akishuhudia utiaji wa Saini ya Maelewano (MoU) kuhusu mpango mkuu wa Ujenzi wa Bandari na Mji wa Kisasa Mangapwani na Bumbwini Zanzibar.(kulia kwa Rais) Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Ndg. Amour Hamil Bakari na (kushoto kwa Rais) Mkurugenzi Mkuu wa Oman Investment Authority (OIA) Sheikh.Mohammed Al Taooqi, hafla hiyo i8mefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza baada ya kumalizika utiaji wa Saini Hati ya Maelewano (MoU) ya ujenzi wa Bandari ya Mwangapwani na ujenzi wa Mji wa Kisasa Bumbwini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mwanasheria Mkuu Zanzibar.Dkt. Mwinyi Talib Haji na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhe.Rahma Kassim Ali, wakifuatilia hutub ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, baada ya kumalizika zoezi la utiaji wa saini ya maelewano ya Ujenzi wa Bandari Mangapwani na Mji wa Kisasa Bumbwini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

No comments: