Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo, akipewa ufafanuzi na Mkurugenzi wa kiwanda cha Chilambo General Tradingcompany Bwa. Gidion Chilambo, namna wanavyofanya shughuli zao kiwandani hapo, kilichopo Kisarawa Mkoa wa Pwani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa kiwanda cha Chilambo General Tradingcompany Bwa. Gidion Chilambo wakati wa ukaguzi katika kiwanda.
Sehemu ya bidhaa chakavu za kielektroniki zitakazo chakatwa na kugeuzwa kuwa malighafi ya bidhaa nyingine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo, akitoa maelekezo baada ya kufika kiwanda cha Prayosha Industries Limited kilichopo Kisarawe Mkoa wa Pwani.
Mhe. Jafo amefanya ziara katika kiwanda hicho kujionea namna wanavyofanya shughuli zao bila ya kuathiri mazingira na kama wanatekeleza sheria ya mazingira ya 2004 na kanuni zake.
Aidha amesema kuwa kiwanda cha Chilambo General Trade company kinasaidia kusafisha mazingira kwa kukusanya taka zote za kielektroniki ili zisiweze kusambaa hovyo mitaani na kurejelezwa kutengeneza bidhaa nyingine. Vile vile amesema kuwa japo kinasaidia lakini wahakikishe wanafanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria ya mazingira
“Ofisi ya mazingira ipo tayari kuwapa msaada na muongozo kuhakikisha viwanda vyao vinasimama pamoja na kuwapa vibali ambavyo itawasaidia kufanya shughuli zao bila bugudha wala uchafuzi wowote wa Mazingira”.Mhe. Jafo
Ameendelea kusema kuwa wawekezaji wote wanaotaka kufanya shughuli ya namna hii wataendelea kupewa miongozo ya kimazingira juu ya namna gani watafanya shughuli zao bila ya kuathiri mazingira.
“Chilambo General Trade Company inatarajia kuanzisha kiwanda kipya cha kurejeleza taka za kielektroniki lakini wanatakiwa kuhakikisha wanakamilisha mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) kwa lengo la kuujua vizuri mradi na athari za kimazingira kabla ya kuanzisha mradi, hii itasaidia kuepusha uingizwaji wa taka ambazo hazitafaa kwa matumizi ya kiwanda.” Mhe.Jafo alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha Chilambo General Trade company amesema kuwa kiwanda kinazingatia sheria ya mazingira na wanacho cheti cha mazingira ila kwa kiwanda wanachotarajia kufungua watafanya Tathmini ya kimazingira kama alivyoagiza Mhe. Waziri Jafo ili kuepusha uchafuzi wa mazingira.
Vile vile Mhe. Jafo ametembelea kiwanda cha Prayosha Industries Limited kinachozalisha malighafi ya sabuni kilichopo Kisarawe Mkoani Pwani kujionea hali ya kimazingira na amekipongeza kiwanda hicho kwa kuzingatia sheria ya mazingira.
No comments:
Post a Comment