Monday, April 18, 2022

SIMBA YATUMIA UWANJA WA NYUMBANI VIZURI


Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa ya kombe la Shirikisho barani Afrika CAFCC, Simba Sc imeendelea kuutumia vema uwanja wa nyumbani wa Benjamin Mkapa a.k.a Lupaso baada ya kuifunga timu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini bao 1-0 katika pambano la kwanza la robo Fainali ya CAFCC lililopigwa Aprili 17, 2022.

Bao pekee lililoipa Simba Ushindi huo muhimu liliwekwa kimiani kwa njia ya mkwaju wa Penati iliyofungwa na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe.

Maamuzi aliamiru penalti ipigwe baada ya Bernard Morrison kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake