Afisa Huduma TRA Mkoa wa Kagera, Alex Mwambenja.
Na Lydia Lugakila
Wafanyabiashara Mkoani Kagera wametakiwa kufuata taratibu za kufunga biashara ili kuepuka kudaiwa kodi za vipindi vilivyobakia katika nwaka.
Kauli hiyo imetolewa na Alex Mwambenja ambaye ni Afisa huduma TRA mkoa wa Kagera akikazia juu ya tangazo la kitaifa
Bwana Alex amesema kuwa wafanyabiashara wanapotaka kufunga biashara wanatakiwa kufuata taratibu za kufunga biashara zao ikiwa ni pamoja na kupeleka barua TRA juu ya kufunga biashara hiyo na kuhakikisha imethibitishwa na serikali ya mtaa husika.
Aidha katika hatua nyingine Mwambenja amesema kuwa mfanya biashara atatakiwa kuhakikisha anarejesha cheti cha TIN cha biashara katika ofisi ya TRA na kuwa kwa kufanya hivyo kutamsaidia mfanyabiashara kutodaiwa kodi za vipindi vilivyobakia katika mwaka.
No comments:
Post a Comment